Halmashauri ya Wilaya Masasi ilianzishwa March 1958 kipindi ambacho ilifanikiwa kuanza kazi mnamo July 1972 ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipoanzisha serikali za Mitaa (Decentralization programme). Ambapo imeanishwa katika sheria namba 07 ya 1982. Halmashauri ya Wilaya Masasi ni miongoni mwa Halmashauri tisa (9) zinazounda Mkoa wa Mtwara.
Halmashauri ya Wilaya Masasi imejumuisha Idara na vitengo tofauti ili kuwezesha kupatikana kwahuduma kiurahisi katika Halmashauri ya Wilaya Masasi.
HISTORIA YA KITENGO CHA UGAVI & MANUNUZI.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi kilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ilitungwa na kusimamiwa kwa sheria ya mwaka 2011(Public Procurement Act 2011) na kanuni zake The Public Procurement Pegulations,2013, iliyofanyiwa malekebisho mnamo mwaka 2016, Government Notice NO.446; imeelezea maana halisi ya ugavi na manunuzi kuwa ni shughuli zote zinazofanywa za ukununua ,kukopa/kuazima na kuuza kwa mujibu wa sheria kama ilivyooanishwa katika sheria na kanuni zilizopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
DIRA NA MWELEKEO.
Dira ya kitengo cha ugavi na manunuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ni upatikanaji wa Wazabuni wa uhakika anaeweza kuwa na huduma stahiki, zenye ubora halisi kwa bei halisi ya bidhaa zitakazotokana na ushindani wa wazabuni wenye sifa. Kuwa na Wazabuni wenye sifa za kiushindani, kiuchumi, mwajibikaji, kutoka na Uuzaji, usambazaji na huduma zingine zitakazoitaji huduma kutoka kwa wazabuni husika katika ununuzi na ugawaji. Kua na usawa wa huduma kwa Wazabuni katika kutekeleza, haki usawa, kiushindani na uwazi katika kutimiza tija na Malengo katika Idara zingine ndani yana Nje ya Halmashauri ya Masasi kulingana na sharia na kanuni elekezi za Ugavi na Manunuzi. The Public Act, Act NO.7 of 2011 and The Public Procurement Regulation,2013, Government Notice NO, 446.
MWELEKEO
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi katika kitengo cha Ugavi na Manunuzi kina mwelekeo mzuri katika utekelezaji wa sheria za Manunuzi na Ugavi kama zilizoanzishwa kwa mujibu wa sharia ya 2011 na kanuni zake za mwaka 2013 na marekebisho yake ya mwaka 2016 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwelekeo wa kitengo cha Ugavi na Manunuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kimejikita pia katika maeneo yafuatayo mbali na sheria ya Ugavi na Manuuzi nayo ni:-(Procurement Act and Regulation);
Uchumi na Utumiaji sahihi wa fedha ya Umma
Kuwa na usawa kwa Wazabuni wote na Utekelezaji sawa kwa Idala
Uadilifu katika Utendaji
Uwazi wa Taarifa na Uwajibikaji katika kitengo cha Manunuzi.
Uzingatiaji thamani ya fedha na uhalisia wa bidhaa husika,
Malengo ya kitengo katika utoaji wa huduma
Halmashauri ya wilaya Masasi katika kitengo cha Ugavi na Manunuzi kina malengo yafuatayo katika utoaji wa huduma.
Kukusanya takwimu za kusaidia kutayarishwa makisio ya Mahitaji yanayohitajika (Procurement Plan) na mpango wa ununuzi
Kukusanya na kutunza takwimu za utendaji wa wazabuni mbalimbali
Kukusanya na kutunza takwimu za upokeaji utunzaji na usambazaji wa vifaa.
Kusimamia upatikanaji, mtunzaji na usambazaji wa vifaa (physical distribution)
Kutayarisha taarifa za kazi katika vipindi maalum.
Kuhesabu na kutoa taarifa ya thamani ya vifaa vilivyopo kila mwisho wa mwaka (Amount stock taking)
Kufanya kazi za tunazopangiwapangiwa
VITENGO VILIVYOPO KWENYE IDARA NA MAJUKUMU YAKE.
Halmashauri ya wilaya masasi imeundwa na idara tofauti tofauti. Idara ya Utumushi pia imebeba jukumu la kusimamia kitengo cha ugavi na manunuzi, hivyo kwa mujibu wa muundo kazi katika halmashauri ya wilaya masasi kitengo cha ugavi na manunuzi kinafanya majukumu yake kwa mujibu wa sharia ya manunuzi ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013 na marekebisho ya mwaka 2016 Na jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MAJUKUMU YA KITENGO KWA UJUMLA
Kitengo cha ugavi na manunuzi kwa ujumla kina jukumu la kusimamia shughuli zilizopo kwa mujibuwa sharia na kanuni zake katika kutoa huduma kwa Umma, wazabuni na idara ama vitengo vinavyoshirikiana navyo katika kutoa huduma hizo.
AINA ZA HUDUMA MUHIMU ZINAZOTOLEWA KWA JAMII MARA KWA MARA.
Kuleta utafiti na kutoa ushauri jinsi gani gharama za ununuzi au utunzaji wa vifaa zinaweza kupunguzwa.
Kutathimini vifaa vinavyotumiwa na idara mbalimbali ilikujua aina na kasi ya matumizi ya vifaa husika kwa hatua Zaidi
Kutayarisha makisio ya vifaa vinavyohitajika (material reguirementBudgent)
Kutayarisha mpango wa ununuzi (reocumener plan)
Kushauri juu ya sera ya ununizi na ugavi serikalini