Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji ni idara inayohusika na masuala ya Kuratibu Mipango yote, Utekelezaji, Usimamizi na tathmini ya miradi ya Maendeleo katika halmashauri pamoja na kuandaa za bajeti ya Halmashauri.
Idara ya Mipango pia inashughulika na Kuandaa taarifa za utekelezaji kwa kila robo ya mwaka ikihusisha taarifa ya miradi,fedha na hatua za utekelezaji. Kuandaa taarifa ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama kwa Kila miezi sita, Kuandaa taarifa za Mafanikio za Serikali iliyoko madarakani, Kuandaa Mpango kazi wa utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo (Action Plan) na Kutoa taarifa za fursa za uwekezaji ndani ya Halmashauri.
USIMAMIZI WA MIRADI.
Idara ya mipango kwa kushirikiana na idara zenye miradi inawajibika kusimamia miradi kuanzia ngazi ya halamashauri hadi ngazi ya vijiji kwa kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara wa miradi hiyo. Utekelezaji wa miradi katika halmashauri inatokana na vyanzo mbalimbali vya fedha ikiwemo ruzuku serikali kuu, mapato ya ndani na wahisani.
CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI WA MIRADI
Ucheleweshwaji wa fedha za miradi ya maendeleo hali inayopelekea miradi kutokamilika kwa wakati, Ushiriki hafifu wa Wananchi katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo, Wananchi kutokulipa kipaumbele zoezi la kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa