CHIPUTULA: TUMEKUJA IRAMBA KUJIFUNZA KWA VITENDO NAMNA BORA YA UKUZAJI NA UKUSANYAJI WA MAPATO ILI HALMASHAURI ZETU ZIWE VINARA KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO.
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara katika kuhakikisha inaongeza nguvu ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa Wananchi wake imeanza ziara yake ya kimafunzo katika maeneo mbalimbali ili kujifunza kwa vitendo namna bora ya uzalishaji na usindikaji wa mazao ya alizeti, ufuta, karanga na mbaazi.
Ziara hiyo ya siku Saba ambayo imeanza tangu tarehe 01 /12/2024 pia imelenga pia ujifunzaji na kubadilishana uzoefu kuhusu masoko, ukusanyaji wa ushuru na tozo kutokana na mazao hayo ya alizeti, ufuta mbaazi na karanga, huku suala la usimamizi na utaratibu wa ukusanyaji wa ushuru na tozo kutokana na madini ya ujenzi nalo limepewa kipaumbele
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida ndipo ziara hii imeanzia ambapo waheshimiwa Madiwani wakiambatana na Mkurugenzi Mtendaji Bi.Beatrice Mwunuka, pamoja na wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wamejifunza kuhusu upatikanaji wa mbegu, Elimu ya ugani, uandaaji wa mashamba, masoko, viwanda vya kusindika, mnyororo wa thamani wa zao la alizeti, kutembelea Wakulima, kukutana na Vikundi vya wajasiriamali wa bidhaa zinazotokana na zao la alizeti pamoja na wajasiriamali wa mafuta.
Mhe.Ibrahimu Chiputula ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi pamoja na kuushukuru Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwa mapokezi mazuri na kuungana nao kwa muda wote pia amesema kwamba "tumekuja hapa Iramba na msafara huu kuja kujifunza Kwa vitendo, Mkurugenzi wetu Bi.Beatrice Mwinuka alituambia tuje Iramba na tumeona ni Kweli vitu vinafanyika, mpo vizuri sana hongereni sana."
Amesema Halmashauri yenye mapato ndio Halmashauri ambayo inakuwa na nguvu ya kutekeleza miradi kwa Wananchi na kuondoa kero za Watanzania hivyo wamefika katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kuongeza maarifa waliyonayo ili wasonge mbele na nina imani kubwa haya tuliyopata hapa tutakwenda kuyatumia vizuri na Halmashauri yetu itapanda katika suala la mapato "....alisema Chiputula
Kwa upande wake Mhe.Innocent Msangi ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida pamoja na Mambo mengine amemshukuru Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa kuwa na maamuzi ya kufika Iramba kujifunza ambapo pamoja na mengine wao wamefurahishwa sana kwasababu kitendo hicho kwao Kama Halmashauri kimewaheshimisha sana na kuonyesha undugu wa dhati.
"Kwakwelii nimejawa na furaha sana kutembelewa Iramba na Halmashauri Nyingine kutoka Mkoa wa Mtwara Masasi ,tangu niwe hapa Kama mwenyekiti sijawahi kupata ugeni Kama huu kwangu ni heshima kubwa, hongera sana Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kuchukua maamuzi haya"
Hata hivyo kesho Tarehe 04/12/2024 ziara hiyo itaendelea katika Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara na kisha kuelekea Chalinze Mkoani Pwani.
03/12/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa