Kamati ya Ushauri Wilaya (DCC) Wilayani Masasi Mkoani Mtwara leo tarehe 19/11/2024 imeketi na kuridhia kwa pamoja pendekezo la kubadilishwa Jina la tarafa ya Lisekese, kuwa sasa Jina jipya ni tarafa ya Lukuledi na makao makuu yake ni Kata ya Chiwale.
Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Wilaya ya Masasi mhe.Lauter Kanoni imefikia maamuzi hayo baada ya kufanyika kwa vikao mbalimbali vya maamuzi vilivyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi na kikao cha Maendeleo ya tarafa Cha tarehe 19/08/2024 ambacho kilipendekeza ujenzi wa Ofisi na nyumba ya Afisa tarafa ijengwe katika Kata ya Chiwale kwa kuwa pamependekezwa kuwa makao makuu ya Tarafa ya Lukuledi.
Awali akisoma taarifa ya mapendekezo ya kubadilisha Jina la Tarafa ya Lisekese na kupitisha makao makuu ya Tarafa hiyo Bi. Irene Mbwana ambaye ndiye Afisa tarafa ya Lukuledi (awali ilikuwa Lisekese) ameelezea kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya Mwaka 2022, Kata yenye watu wengi ni Kata ya Chiwale yenye jumla ya watu wapatao 21,466 na Kata yenye watu wachache ni Kata ya Chikunja yenye Jumla ya watu 6,423.
Amesema kwamba pamoja na Shughuli kuu za kiuchumi ni Kilimo cha mazao biashara Kama korosho, ufuta, mbaazi, na mazao ya chakula Kama vile mahindi na muhogo huku baadhi ya Wananchi wakijishughulisha na biashara ndogo ndogo, pia sababu Nyingine ya pendekezo hilo ni kutokana na jiografia ya Kata ya Chiwale ambayo ipo katikati ya Kata zote 8 zilizopo katika Tarafa hiyo na inafikika kwa urahisi kutokea katika Kata zote.
"Kata ya Chiwale pia ina eneo la kutosha lenye uwezo wa kuruhusu ujenzi wa majengo mbalimbali ya Serikali Kama vile Ofisi ya Tarafa, Mahakama,nyumba ya Afisa tarafa, soko na kituo Cha polisi hivyo kubadilisha Jina la tarafa ya Lisekese kuwa Tarafa ya Lukuledi, tufahamu kuwa Tarafa ya Lisekese haina kijiji Wala Kata inayobeba Jina la tarafa ya Lisekese Kama ilivyo kwenye tarafa zinginge kama Lulindi, Chiungutwa na Machauru".
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe walioshiriki kwenye kikao hicho cha Kamati hiyo ya Ushauri Wilaya (DCC) wamepongeza hatua hiyo waliyofikia ya maelewano katika maeneo ya utawala ambapo wamejadiliana kwa amani na mwisho wa siku wametoka na wazo Moja ambalo linaendelea kuweka historia kwa Jamii hususani kutumika Jina la tarafa ya Lukuledi kwasababu kwenye Kata ya lukuledi upo mto ambao unapakana na Wilaya ya Nachingwea na Masasi hivyo kuitwa Tarafa ya Lukuledi ni heshima kwako.
Katika hatua nyingine Kamati hiyo ilipokea pia taarifa ya mrejesho wa Kitongoji cha Singino kilichoomba kuhamishiwa katika Kijiji Cha chikundi kutoka Katika Kijiji Cha Msigalila.
Kwa vipindi tofauti tofauti vikao mbalimbali vya kisheria vilikaa na kujadili ambapo kikao cha Tarehe 18/04/2023 kiliridhia ombi la kitongoji Cha Singino kuhamia katika Kijiji Cha Chikundi na kikao cha Maendeleo ya Kata (WDC) ya Kata ya Chikundi cha tarehe 23/05/2023 kwenye ajenda Na.02/MAY/WDC/2023 iliridhia ombi la kitongoji Cha Singino kutoka Kijiji Cha Msigalila kwenda Kijiji Cha Chikundi.
Hata hivyo Kwa mujibu wa tangazo la Serikali Na.796 lililotolewa kwenye gazeti la Serikali Na 32/VOL.105 la tarehe 06/09/2024 Kutoka OR-TAMISEMI iliridhia maombi ya kitongoji Cha Singino kuhama Kutoka Kijiji Cha Msigalila kwenda Kijiji Cha Chikundi katika Kata ya Chikundi.
19/11/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa