1.ASILI YA NENO MASASI
UTANGULIZI
Kwa sasa Masasi ni moja ya wilaya tano zinazounda Mkoa Mtwara, ipo umbali wa kilomita 199 kutoka Mtwara mjini. Kiramani, Masasi imepakana na mto Ruvuma upande wa kusini, magharibi imepakana na mto Lukuledi na mashariki ikipakana na Uwanda wa Juu wa Umakonde. Unaambiwa hivi, ukisikia jina Masasi huwa kuna vitu vinawakilishwa, yaani kuna Masasi mlima,
Wilaya ya masasi ina Halmashauri mbili yaani Masasi wilaya na Mji. Ukiwa katika Halmashauri ya wilaya ya Masasi ina kata 34 zikiwemo Chigugu, Chiungutwa, Lipumburu ,Lukuledi, Lulindi ,Mbuyuni, Mchaura ,Mkululu, Mkundi, Mnavira, Mpindimbi, Mwena Namajani ,Namalenga, Namatutwe, Nanganga ,Nanjota, Sindano n.k
ASILI YA NENO MASASI
Kihistoria hapo mwanzoni, Masasi kulikuwa na mapori tu, yaliokuwa na simba na wanyama wengine wa porini. Lakini miaka ya 1400 makundi ya wabandu waliofahamika kama Wandonde walifika kwenye maeneo hayo. Hivyo kabla ya ujio wa Wamakua Masasi ilifahamika kwa jina la Undonde, lakini mnamo miaka ya 1700 mpaka 1800 katika ardhi ya Wandonde wakaingia wakazi wapya kutoka Msumbiji waliofahamika kama Wakamkua. Wamakua walikaa hapo na ndio wakazi maarufu kwenye wilaya ya Masasi kwa sasa.
Miaka ya 1840 baada ya kukua kwa biashara ya utumwa na biashara zingine, kwenye ardhi ya Masasi kukawa na ujio wa wageni ambao ni Waarabu waliofika hapo kama wafanyanbishara. Miaka ya 1850-1890 maeneo ya Masasi wageni kutoka Ulaya kuanzia wale wamishionari mpaka wakoloni wenyewe waliingia.
Asili ya jina MASASI, kama nilivyokwishafafanua hapo mwanzo kuwa kabla ya maeneo ya Masasi kuitwa Masasi palifahamika kama Undonde na hii ni kutokana na wakazi wa kwanza walifahamika kwa jina la Wandonde. Lakini mara baada ya ujio wa Wamakua na Wayao ndipo kulipozaliwa jina la Masasi.
Hivyo jina Masasi lina mahusiano makubwa sana na Wamakua na sio Wandonde . Inafafanuliwa kuwa neno Masasi linatokana na neno la kimakua “Machasi” likiwa na maana ya “masuke ya mtama”. Kwani miaka ambayo Wamakua wanafika hapo kwenye mlima wa Masasi kulikuwa kunalimwa sana mtama ambayo ulikuwa unastawi sana.
Kutokana na neo hilo ndipo kukazaliwa maneno kama “Umachasini” na wengine kufupisha na kupata “Umachasi” na “Machasi”. Lakini kutokana na ujio wa wageni mbalimbali katika Mji wa Masasi kulizuka matamshi mapya ambayo yalipelekea kuzaliwa kwa neno masasa ktokana na urahisi wa kutaja.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa