1.1. UTANGULIZI
Idara ya Ardhi na Maliasili ni miongoni mwa idara 13 za Halmashauri ya Wilaya Masasi. Idara ina
vitengo viwili ambavyo ni Ardhi na Maliasili
MAJUKUMU/KAZI ZA IDARA ZA KILA KITENGO
2.1. Kitengo cha Ardhi
Majukumu ya kitengo cha Ardhi ni pamoja na kuandaa mipango ya uendelezaji, kusimamia uendelezaji wa mji, kusimamia milki na kufanya uthamini wa ardhi na mali sisizohamishika.
Ili kute kutekeleza majukumu hayo,kiengo kimegawanyika katika sehemu kuu nne kama inavyoelezwa hapa chini.
(a) Mipango Miji;
• Kusimamia uandaaji wa Mpango Kamambe wa mji (Master plan)
• Kuandaa mipango ya kina ya uendelezaji wa ardhi katika maeneo ambayo yameiva kwa
uendelezaji ili ujenzi wake ufuate taratibu na sheria za mipangomiji
• Kuandaa mipango maerekebisho ya michoro ya mipangomiji (Amendment Schemes)
Kuandaa mipango ya uboreshaji maeneo yaliyojengwa holela (Regularazation/Upgrading
Schemes)
• Kutoa masharti ya undelezaji wa ardhi
• Kusimamia uendelezaji wa mji wa kila siku (urban development control)
• Kuchunguza ramani za Majengo kwa ajili ya utoaji vibali vya ujenzi.
• Kutoa ushauri wa uendelezaji wa ardhi kwa wananchi.
(b) Upimaji na Ramani
• Kulinda na kusimamia sheria za upimaji ardhi kwa mujibu wa sheria za upimaji ardhi (sheria namba 390 ya mwaka 1956
• Kutoa maelekezo ya upimaji
• Kupima viwanja vya matumizi mbalimbali na mashamba
• Kupima mipaka ya vijiji
• Kufanya upimaji kwa ajili ya ramani za kihandisi (Topographical Survey, Base Maps
etc)
• Kuchora ramani za Hati (Deed Plan)
• Kuweka alama za msingi (Control Points)
• Kutoa ushauri wa wananchi juu ya upimaji/faida za upimaji
• Kutoa ushahidi mahakamani kwa kesi mbalimbali zinazohusu matatizo ya mipaka na
uvamizi
• Kutatua migogoro ya mipaka ya viwanja na mashamba
• Kufufua na kurudishia alama za mipaka
• Uchoraji na utayarishaji ramani za viwanja
• Kutoa ushauri na kutunza kumbukumba za upimaji ardhi.
c) Usimamizi wa Ardhi
• Kushughulikia maombi ya viwanja na ugawaji wake
• Kutayarisha barua za toleo kwa wamiliki
• Kuhamisha miliki na kurejesha (Surrender)
• Kusimamia masharti yaliyokuwemo katika hati miliki
• Kuandaa na kuratibu mapendekezo ya ufutaji wa viwanja, uhawilishaji
• Kushughulikia migogoro ya ardhi
• Kutoa ushauri kwa wananchi kwa masuala yahusuyo milki za ardhi
• Kutunza kumbukumbu za milki
• Kuandaa na kusajili leseni za makazi
• Kusajili mikopo kwa taasisi na watu binafsi kwa kutumia leseni za makazi na Hatimiliki za kimila
• Kusimamia na kutoa vibali vya mauziano ya leseni za makazi
• Kupokea maombi ya kubadili matumiza ya ardhi
(d) Uthamini
• Kukadiria kodi za viwanja/mashamba
• Kukagua na kukadiria kiasi cha malipo ya fidia ya mali za wananchi kwenye utwaaji
wa ardhi
• Kutoa thamani ya mali kabla ya kuidhinisha mabadiliko ya milki
• Kutoa thamani katika mahakama kwenye shauri za mirathi, mngawanyo wa mali
kwenye mirathi na wanandoa
• Kukadiria thamani ya Majengo kwa ajili ya mikopo toka taasisi za fedha
• Kutoa thamani ya mali kwa ajili ya hesabu, kumbukumbu za mali,mizania nk
• Kukadiria/kushauri kodi za pango (House rent)
• Kutoa ushauri wa uanzishaji na aina za miradi
• Utafiti wa viwango vya gharama za ujenzi na kodi za ardhi
2.2. Kitengo cha Maliasili
Majukumu ya kitengo cha Maliasilini pamoja nakusimamia uhifadhi na utunzaji wa maliasili pamoja na misitu iliyopo katika Halmashuri ya Wilaya Masasi.
Ili kute kutekeleza majukumu hayo,kiengo kimegawanyika katika sehemu kuu nne kama inavyoelezwa hapa chini.
(a) Misitu;
(b) Wanyamapori;
3.0 MIRADI INAYOTEKELEZWA NA IDARA
3.1 Urasimishaji wa Mashamba
Idara inatekeleza miradi ya Urasimishaji wa Mshamba ya wananchi katika vijiji ……………
Urasimishaji wa mashamba ya wananchi unafadhiliwa na taasisi mbi ,Mkurabita na Concern Wordwide.Urasimishaji umegawanyika katika sehemu zifuatazo;
(a) Ujenzi wa masijala za Ardhi;
(b) Uandaaji wa Mpango wa Matumizi bora ya Ardhi;
(c) Uandaaji na utoaji wa Hatimiliki za Kimila;
3.2 Mradi wa Upimaji na Uuzaji wa Viwanja
Idara kwa kushirikiana na Halmashauri ilibuni mradi wa upimaji wa viwanja ili kuongeza idadi ya viwanja
vilivyopimwa, kuzuia ujenzi wa kiholela na kupunguza urasimu katika ugawaji wa viwanja.
Katika kutekeleza hili michoro ya mipango miji imeandaliwa ikiwa na jumla ya viwanja 830 vya matumizi mbalimbali katika eneo la mradi wa upimaji viwanja Ndanda.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa