Jumla ya Vikundi vya wajasiriamali 60 vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu Halmashauri ya Wilaya Masasi Mkoani Mtwara wanatarajia kunufaika na mkopo usio na riba wa tshs. Milioni 700 kupitia asilimia 10% ya mapato yake ya ndani huku Lengo kubwa ni kuviwezesha Vikundi hivyo ili viweze kujiajiri kupitia Shughuli zao za kiuchumi.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na kitengo Cha habari na mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya Masasi, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii ya Halmashauri hiyo Bw.Rashidi Njozi Mussa amesema kwamba mpaka sasa tayari jumla ya vikundi ambavyo vimefanikiwa kuingiza maombi ya mikopo kwenye mfumo vipo Vikundi 60 vyenye thamani ya shilingi Milioni 700, na Kwa wale ambao tayari wameshaomba wamewaandikia Watendaji wa kata kwa ajili ya kuanza kuchambua maombi hayo kwenye kata zao na hatmaye wawaletee wao ngazi ya Halmashauri nao wachambue maombi hayo.
Amesema "tunatamani kabla ya tarehe 30/11/2024 Vikundi vile ambavyo vitakuwa vimekidhi mahitaji yanayotakiwa kunzia ngazi ya kata, Halmashauri pamoja na ile Kamati ya uhakiki ya Wilaya, tuwe tumewapatia mikopo ili waendelee na shughuli zao, lakini Cha msingi vikundi hivi sasa ambavyo tutavikopesha viende vikafanye shughuli iliyokusudiwa na kama kutakuwa na mabadiliko ya mradi basi ni vyema muwasiliane na Ofisi ya Maendeleo ya Jamii ili kujua ni nini kinatakiwa kufanyika, sio mtu anajiamlia tu kwasababu wakija wakaguzi kukagua watasema ni miradi hewa kumbe kuna mtu anajiamlia na kujitengenezea mradi wake"..alisema Bw.Njozi
Aidha Bw.Njozi ameendelea kuelezea kwamba kwa wale wote watakaokopa na ambao wengine tayari walikopa katika siku za nyuma na bado wanadaiwa watambue kuwa Sheria ipo ambayo inawabana wakopaji na wakati mwingine inapelekea kuchukua hata vile vitu walivyokopa mfano pikipiki ili kuwashinikiza walipe, hivyo ili kuepuka kufikia hatua hiyo mkopaji anatakiwa kutii sheria bila shuruti kwasababu mwishowe kupitia sheria ndogo ya fedha ya mwaka 2018- 2019 inawaelekeza mkopaji akishindwa kurehesha mkopo impeleke mahakamani.
"Nasisitiza baada ya kupata mikopo hii tuwekeze kwenye biashara za kiuchumi na tukumbuke kufanya marejesho ili kuwapa fursa watu wengine wapate mikopo hiyo nayo iwasaidie kiuchumi".
Hata hivyo ifahamike kuwa kwa mujibu wa muongozo vipo viwango mbalimbali vya kukopa ikwemo kikundi kinaweza kukopa fedha kuanzia shilingi laki tano hadi shilingi Milioni 10, kundi la pili linaweza kukopa Shilingi Milioni 10 hadi shilingi Milioni 50, na kundi la tatu wanaweza kukopa Shilingi Milioni 50 hadi shilingi Milioni 150.
@masasidc
17/11/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa