Idara ya kilimo, Umwagiliaji na Ushirika ni moja kati ya Idara 13 za Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Awali kabla ya mwaka wa fedha wa 2013/2014 Idara hii ilijulikana kama Idara ya Kilimo, Maendeleo ya Mifugo na Ushirika ambapo Mkuu wa Idara alijulikana kama DALDO, kwa maana ya ‘District Agriculture and Livestock Development Officer’.
KAZI/ MAJUKUMU YA IDARA
Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika ni moja ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya inajishughulisha na kumsaidia/ kumshauri Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Katika mambo yafuatayo:
1. Kuandaa mipango na bajeti ya miradi mbalimbali ya maendeleo ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika.
2. Kuratibu , Kutathimini na kufuatilia shughuli za huduma za ugani wilayani.
3. Kusimamia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji, maghala na masoko wilayani.
4. Kutoa elimu na kuhamasisha wakulima juu ya usimamizi na uendeshaji wa miradi ya umwagiliaji kwa maendeleo endelevu kwa kushirikiana na wadau wengine.
5. Kuongeza uzalishaji na tija kutokana na matumizi ya teknoloji bora zilizopatikiana.
6. Kuongeza ufanisi kwa kutumia zana bora zilizotokana na utafiti.
7. Kuzalisha aina za mbegu za daraja la kuazimiwa zenye mavuno mengi na bora ambazo pia zinastahimili ukame na visumbufu vya mimea na mazao.
8. Kushirikiana na wadau mbalimbali wanaojihusisha na utaafiti wa kilimo, Umwagiliaji na Ushirika na matumizi ya teknolojia husika.
9. Kuandaa taarifa na takwimu mbalimbali za maendeleo ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika.
10. Kuhamasisha kuwepo kwa viongozi wa ushirika wanaowajibika kwa wanachama na ambao ni wabunifu kibiashara.
11. Kujasirisha wanachama kwa kuwawezesha kupata elimu na stadi zinazohitajika ili waendeleze vyama vyao.
12. Kufanya ukaguzi wa hesabu za ndani za vyama vya ushirika na Saccos wilayani
13. Kuhimiza na kuhamasisha uanzishwaji na uendelezaji wa vyama vya ushirika vyenye nguvu za kiuchumi na endelevu.
14. Kuhimiza na kuwezesha mabadiliko katka mfumo wa vyama Ushirika vya Akiba na Mikopo na Benk za Ushirika ili vyombo hivyo viweze kuwahudumia wanachama kikamilifu.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa