TARATIBU ZA KUHAMISHA MWANAFUNZI KUTOKA SHULE MOJA KWENDA NYINGINE NDANI NA NJE YA WILAYA
Uhamisho wa mwanafunzi kutoka shule moja ya sekondari kwenda nyingine hufanywa wakati wa likizo tu isipokuwa kama kuna tatizo kubwa linasababisha uhamisho kufanyika na kwamba asipohamishwa hawezi kusoma au kufuatilia vizuri masomo yake. Aidha uhamisho hutakiwa kufanywa na mzazi au mlezi na sio mwanafunzi mwenyewe.
Ziko aina mbili za uhamisho;-
Uhamisho kutoka shule za sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Masasi kwenda ndani na nje ya Halmashauri .
Uhamisho huu hufanya kwa kuandika barua ya ombi la uhamisho kwa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara na barua kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wilaya, Afisa Elimu Sekondari Wilaya, Mkuu wa shule anakotoka mwanafunzi na Mkuu wa shule anakokwenda mwanafunzi. Mwonekano wa anuani za barua ni kama ifuatavyo;-
Katibu Tawala (M)
S.L.P 544
MTWARA
K.K. Mkurugenzi Mtendaji (W)
S.L.P 60
MASASI
K.K. Afisa Elimu Sekondari
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi
S.L.P. 60
MASASI
K.K. Mkuu wa shule (anakotoka Mwanafunzi. Huyu atapitisha na kujaza fomu za uhamisho)
S.L.P
…………………………….
K.K. Mkuu wa Shule (Anakotaka kuhamia mwanafunzi. Huyu ataonesha kama nafasi ipo ya
kumpokea)
S.L.P
……………………………….
Ili uhamisho uweze kukamilia ni lazima Mzazi/mlezi apate ridhaa kutoka kwa mkuu wa shule anakohamia mwanafunzi hivyo ni lazima barua ya maombi ya uhamisho ipite kwanza kwa mkuu wa shule anakohamia mwanafunzi kwa uthibitisho wa kupata nafasi.
Uhamisho kutoka shule za sekondari zilizo nje ya Halmashauri kuja katika shule za sekondari za halmashauri ya wilaya ya Masasi.
Uhamisho huu hufuata anuani kama zilivyo hapo juu katika uhamisho aina ya kwanza ISIPOKUWA anuani hizi uelekezwa kwa Katibu Tawala wa Mkoa au Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya na afisa Elimu sekondari wa Wilaya anayotoka mwanafunzi. Kabla ya kuwasilisha barua katika ngazi za juu kama anuani zinavyoonesha mzazi/mlezi anatakiwa kupeleka kwanza barua kusainiwa kwa mkuu wa shule anayohamia mwanafunzi na kufuata mfululizo wa anuani kama ulivyo kutoka chini. Aidha jukumu la halmashauri katika uhamisho huu ni kumpokea mwanafunzi baada ya kupata kibali cha uhamisho kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa anakohama.