UTANGULIZI
Idara ya Maendeleo ya Jamii ni miongoni mwa Idara 13 na vitengo 6 katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
DIRA YA IDARA: (VISION)
Kuhakikisha jamii inaondokana na janga la umaskini na kujenga jamii yenye fikra ya kujitegemea kiuchumi na kijamii kwa kujishughulisha na shughuli za kiujasiriamali ili kujiongezea kipato
MWELEKEO WA IDARA: (MISSION)
Kuwa miongoni mwa idara inayotoa huduma kwa ubora na ufanisi kwa kujiunganisha, kuisimamia na kuiwezesha jamii ili iweze kufanya shughuli zamaendeleo ili kuondokana na umaskini.
VITENGO NA MAJUKUMU YAKE:
Idara ya Maendeleo ya Jamii ina vitengo vikuu sita (6)
a) Kitengo cha mfuko wa maendeleo ya wanawake (WDF)
b) Kitengo cha kupambana na kudhibiti Ukimwi.
c) Kitengo cha kuratibu Asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s)
d) Kitengo cha mfuko wa maendeleo ya vijana (YDF)
e) Kitengo cha Ustawi wa Jamii.
f) Kitengo cha mipango, ufuatiliaji na utafiti.
MAJUKUMU YA VITENGO VYA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
a) Kitengo cha uratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) na
b) Kitengo cha Uratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF)
Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake na Vijana ni mfuko ya masharti nafuu iliyoanzishwa na serikali kuongeza mitaji kwa Wanawake na Vijana wajasiliamali. Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF), na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) uliyoanzishwa na serikali kwa azimio la Bunge kwa Mujibu wa “exchequer and Audit Ordinance” ya mwaka 1961.
LENGO LA VITENGO VYA WANAWAKE (WDF) NAVIJANA (YDF)
· Kuwezesha kundi la Wanawake na Vijana kupataajira hatimaye kujitegemea kiuchumi na kijamii kupitia mikopo ya masharti nafuu, ambayo huwawezesha kukuza mitaji kupitia kufanya kazi hai za uzalishaji mali, ambapo huondoa utegemezi, wakati huohuo huchangia kukuza uchumi na kuondoa umasikini mahalia, familia na Taifa.
WALENGWA WA MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKE (WDF) WALENGWA WA MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA (YDF).
· Wanawake na Vijana wote wenye uwezo wa kufanya kazi na ambao tayari wanaonyesha jitihada, nia ya kuchangia na pia uzalendo wa kurejesha kwa kadri ya makubaliano, aidha lazima wawe katika kukundi rasmi chenye lengo kinalolingana, vina kazi zenye tija na zenye matokeo, Katiba (Makubalinao kukifanya kuwa endelevu), kuwa na kinachotambulika toka ngazi ya Kitongoji Kijiji, Kata na Wilaya (Kimesajiliwa), kuwa na michanganuo.
BAADHI YA SIFA ZA MIRADI INAYOOMBEWA
c) Kitengo cha Utafiti,Takwimu na Mipango.
Ni kitengo ambacho kinajishughulisha na shughuli mbalimbali;-
i) Kufanya utafiti wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya Jamii na kujenga uelewa kwa jamii kuhusu Fursa na Vikwazo vya Maendeleo (O&OD)
ii) Kukusanya na kutunza taarifa na takwimu mbalimbali za Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya matumizi ya idara.
iii) Kuandaa na kupendekeza mipango na mikakati ya kubadili fikra za watu ili waweze kuwa ana mawazo ya maendeleo sawia na sera za serikali.
iv) Kupanga mipango mbalimbali ya idara kwa ajili ya Maendeleo ya Jamii.
d) Kitengo cha kupambana na kudhibiti Ukimwi
i. Kuhamasisha jamii juu ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI.
ii. Kuhamasisha jamii kuondokana na unyanyapaa.
iii. Kutoa usaidizi katika makundi tete.
e) Kitengo cha Uratibu wa Asasi.
i. Kutoa ushauri kwa NGO’s, CBO’s juu ya uundaji wa katiba uanzishwaji wa vikundi pamoja na ubunifu wa miradi.
ii. Kusimamia na kuratibu Asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) ili ziweze kufanya kazi zake kwa ufanisi.
iii. Kutoa elimu juu ya kuandaa maadhiko ya miradi (Project Proposal) kwa vikundi na mshirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s).
f) Kitengo cha Watoto
i. Uratibu wa mabaraza ya watoto.
ii. Utambuzi wa watoto waishio katika mazingira hatarishi.
MAJUKUMU YA JUMLA YA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
g) Kupitia mbinu shirikishi kuiwezesha jamii kuanzisha miradi ya kijamii kama vile usafi wa mazingira, ujenzi wa nyumba bora, shule, zahanati na majosho.
h) Kuelimisha viongozi wa serikali ya vijiji, dini na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu sera mbalimbali za wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kuhusu sera mbalimbali za wizara.
i) Kuwawezesha wananchi kupambana na mila zenye madhara kwa afya za wananchi hasa kwa wanawake na watoto wa kike, kuenea kwa virusi vya Ukimwi na magonjwa ya mlipuko.
j) Kutoa huduma kwa jamii kwa vipengele vya Ustawi wa Jamii na msaada wa kisaiklojia
k) Kutoa elimu juu ya kupambana na Virusi vya Ukimwi (VVU) na ugonjwa wa Ukimwi pamoja na kutoa msaada kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (inategemea na bajeti)
l) Kuwezesha na kuimarisha shughuli za mfuko wa wanawake na vijana kwa kuvipatia mkopo wa masharti nafuu kwa vikundi vya kiuchumi.
m) Kuratibu maadhimisho ya sherehe mbalimbali za kitaifa.
HUDUMA ZINAZOTELEWA NA IDARA KWA SASA.
Huduma zinazotolewa na Idara ya Maendeleo ya Jamii mara kwa mara ni:
a) Kutoa ushauri kwa NGO’s, CBO’s juu ya uundaji wa katiba na uanzishaji wa vikundi pamoja na ubunifu wa miradi
b) Kuratibu mfuko wa Maendeleo ya Wanawake na Vijana au kuviwezesha vikundi vya wanawake na vijana mikopo ya masharti nafuu.
c) Kuratibu maadhimisho ya sherehe mbalimbali za Kitaifa
d) Kutoa huduma kwa jamii kwa vipengele vya ustawi wa jamii, ushauri na msaada wa kisaikolojia.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa