Watumishi wa Umma Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wametakiwa kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika kikamilifu katika kusimamia miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo inatekelezwa katika Halmashauri hiyo ili fedha zinazotolewa na mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan zitumike Kuleta maendeleo Kwa Wananchi.
Hayo yamesemwa Jana tarehe 19/11/2024 na Mkuu wa Wilaya ya Masasi mhe.Lauter Kanoni mara baada ya kukutana na Watumishi hao kwenye kikao maalumu kilichofanyika katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri hiyo uliopo Masasi mjini huku ajenda kuu ikiwa ni kuwatambua watumishi wapya ambao wamefika katika Halmashauri hiyo (ajira mpya) pamoja na kukumbushana masuala mbalimbali ya kiutendaji wawapo kazini.
Amesema "Serikali ina dhamira ya dhati ya kutuletea Maendeleo kwenye maeneo yetu ndio maana tumeshuhudia fedha nyingi zimeletwa katika Halmashauri ya Wilaya Masasi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika nyanja mbalimbali ikwemo Elimu,Afya, Maji,n.k hivyo ninawaomba sana msimuachie Mkurugenzi peke yake kusimamia hii miradi, nyinyi ndio wasaidizi wake msaidieni kazi Kila mmoja katika eneo lake awajibike kwasababu nyinyi Watumishi mmepewa dhamana ya kuisaidia Serikali kwaiyo nawaomba sana"
Aidha mhe.kanoni ameendelea kuwakumbusha Watumishi hao kuwa wajiandae ipasavyo kuwa na maelezo sahihi juu ya miradi yote inayotekekezwa kwani Kamati yake ya Ulinzi na Usalama Wilaya hivi karibuni itaanza ziara katika Halmashauri hiyo ili kukagua na kuona Maendeleo ya miradi hiyo imefikia wapi,nini changamoto zake na wametatua kwa namna gani kupitia Wataalamu waliopo kwenye Halmashauri hiyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bi.Beatrice Mwinuka pamoja na kumshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kutenga muda na kuzungumza na Watumishi hao pia amekiri uwepo wa kasi ndogo ya ujenzi wa miradi ambayo kwa asilimia kubwa inatekelezwa na wakandarasi na hivyo kuhaidi kuwachukulia hatua ikiwemo kuvunja nao mikataba kwasababu wamekuwa wakiichelewesha miradi hiyo licha ya kukutana nao na kuzungumza nao Mara Kwa mara.
20/11/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa