Dhumuni la kuanzishwa kwa kitengo hiki ni kuhakisha zoezi la uchaguzi wa viongozi mbalimbali kwenye Halmashauri wakiwemo Rais, Wabunge, Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji pamoja na wajumbe wa Halmshauri ya Vijiji linafanikiwa.kitengo hiki kwa kiasi kikubwa hufanya kazi kwa ukaribu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Kitengo cha Uchaguzi cha Mkoa.
Kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya uchaguzi nchini ,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ndiye Msimamizi wa Uchaguzi kwenye majimbo yote yaliyoko kwenye halmashauri yake kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kwa mamlaka aliyopewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi humteua Afisa ambaye hufanya shughuli zote zinazohusiana na Uchaguzi kwenye Halmashauri kwa niaba ya Mkurugrenzi Mtendaji. Afisa huyo ndiye Afisa Uchaguzi wa Halmashauri.
MAJUKUMU YA KITENGO CHA UCHAGUZI CHA HALMASHAURI.
MAJIMBO YA UCHAGUZI.
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ina jumla ya vitongoji 889,vijiji 166 na kata 34 ambazo ziko ndani ya majimbo mawili ya Uchaguzi ya halmshauri ambayo ni Jimbo la Lulindi ambalo lina ukubwa wa sqkm 1961.4 na jimbo la Ndanda ambalo linaukubwa wa sqkm 1868.5.
MIONGOZO ,KANUNI NA SHERIA ZINAZOSIMAMIA UCHAGUZI NCHINI.
Kitengo kinapata nguvu ya kufanya uratibu kwenye masuala yote yahusuyo uchaguzi kwani nchi imejiwekea miongozo, kanuni na sheria mbalimbali zinazotoa mamlaka kwa vyombo vinavyohusika na uchaguzi kutekeleza majukumu yake ambazo ni -
TARATIBU ZA KUPATA VIONGOZI.
Njia pekee itumikayo kupata viongozi nchini ni njia ya kupiga kura na kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Ibara ya 5) inatoa haki kwa kila raia wa Tanzania aliyetimiza miaka kumi na minane kupiga kura katika uchaguzi unaofanywa Tanzania na wananchi. Na haki hii itatumiwa kwa kufuata masharti ya ibara ndogo ya (2) pamoja na masharti mengineyo ya Katiba hii na ya sheria zingine zinazotumika nchini zinazohusu uchaguzi .
Bunge laweza kutunga sheria na kuweka masharti yanayoweza kuzuia raia asitumie haki ya kupiga kura kutokana na yoyote kati ya sababu zifuatazo, yaani raia huyo -
Kuwa na uraia wa nchi nyingine.
Kuwa na ugonjwa wa akili
Kutiwa hatiani kwa makosa Fulani ya jinai
Kushindwa kuthibitisha au kutoa kitambulisho cha umri, uraia au uandikishwaji kama mpiga kura
Pia Bunge litatunga Sheria ya Uchaguzi na kuweka masharti kuhusu mambo yafuatayo –
UCHAGUZI WA RAIS NA WABUNGE .
Kwa mujibu wa katiba ibara ya 38 ,Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa katiba na sheria itakayoweka masharti kuhusu uchaguzi wa Rais ambayo itatungwa na Bunge kwa kufuata masharti ya Katiba.
Kitengo cha Uchaguzi kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi kwenye halmashauri ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji kimepatiwa mamlaka ya kusimamia zoezi la uchaguzi na kubandika matokeo ya uchaguzi ya urais lakini hakina mamlaka ya kutangaza kwani mwenye mamlaka ya Kutangaza matokea ya Uchaguzi wa Rais ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
SIFA ZA MTU KUCHAGULIWA KUWA RAIS ( IBARA YA 39).
Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri wa Muungano isipokuwa tu kama-
Ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia.
Ametimiza umri wa miaka arobaini
Ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa.
Anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.
SIFA ZA MTU KUCHAGULIWA KUWA MBUNGE (IBARA YA 66 NA 67).
Mbunge ni mwakilishi wa wananchi katika Jimbo na mtu yeyote atachaguliwa kuwa mbunge ikiwa atakidhi sifa zifuatazo –
Ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja na ambaye anajua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili au kiingereza.
Ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa
Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.
Msimamizi wa Uchaguzi kwenye halmashauri kupitia kitengo cha Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji amepatiwa mamlaka ya kusimamia zoezi la uchaguzi , kubandika na kutangaza matokeo ya uchaguzi ya Wabunge wa majimbo yaliyopo kwenye halmashauri yaani Jimbo la Lulindi na Jimbo la Ndanda.
UCHAGUZI WA MADIWANI
Diwani ni mwakilishi wa wananchi kwenye kata na pia ndiye mjumbe wa kamati ya maendeleo ya kata.Diwani hupatikana kwa kuchaguliwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano. Msimamizi wa Uchaguzi kwenye halmashauri kupitia kitengo cha Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji amepatiwa mamlaka ya kusimamia zoezi la uchaguzi , kubandika na kutangaza matokeo ya uchaguzi ya Madiwani waliochaguliwa kwenye kata 34 za Halmshauri za Wilaya ya Masasi.
SIFA ZA KUGOMBEA UDIWANI
Mtu yeyote anaweza kugombea na kuchaguliwa kuwa Diwani iwapo anakidhi sifa zifuatazo –
Awe ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Awe ametimiza umri wa miaka ishirini na moja au zaidi
Awe na akili timamu
Awe ni mkazi wa kata husika
Anaweza kusoma na kuandika Kiswahili na kiingereza
Awe ni mwanachamawa wa chama cha siasa kilichosajiliwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, sura ya 25 na chama chake kimemteua akiwakilishe kwenye uchaguzi husika.
Awe na njia halali za kujipatia kipato
Asiwe amehukumiwa kwa kosa la ukwepaji kodi ndani ya kipindi cha miaka mitano kabla ya uchaguzi
Asiwe amehukumiwa kifo au amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita jela.
VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA
Katika vijiji nafasi zinazogombewa ni Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji, wajumbe wa halmashauri ya kijiji na wajumbe wa viti maalumu wanawake, na kati wajumbe watakao chaguliwa idadi ya wanawake itakuwa nusu au zaidi ya wajumbe wote. Idadi ya wajumbe wa kijiji haitazidi ishirini na tano.na kwa kiasi kikubwa Tume ya Uchaguzi huwa haijihusishi na uchaguzi huu na badala yake TAMISEMI humpa mamlaka Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
SIFA ZA WAGOMBEA
Mgombea kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa, vijiji na vitongozi anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo –
WAJIBU WA VIONGOZI KWENYE MAJIMBO, KATA ,VIJIJI NA VITONGOJI
Kila kiongozi atakaechaguliwa na wananchi kupitia uchaguzi anawajibu wa -
CHANGAMOTO ZINAZO KABILI KITENGO CHA UCHAGUZI CHA HALMASHAURI
Kama ilivyoada changamoto huwa hazikosi kwenye kila jamboila kwa ufupi kitengo kinakabiliwa na changamoto kuu mbili –
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa