TANGAZO TANGAZO TANGAZO
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi anapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa serikali imepiga marufuku uingizaji,uzalishaji, usambazaji, uuzaji na utumiaji wa mifuko ya plastiki hapa nchini ifikapo 31 Mei, 2019.
Baada ya tarehe 31 Mei, 2019 serikali itafanya msako kwa watakaokaidi agizo hili. Aidha msako huo utaambatana na utozwaji wa faini na adhabu ya kifungo au vyote kwa pamoja.
Hivyo kila mwananchi azingatie agizo hili ili kutunza mazingira lakini pia kuepuka mkono wa sheria. Kwa watakaokuwa na mifugo ya plastiki waisalimishe kwenye ofisi ya serikali ya kijiji/mtaa/kata kabla ya juni mosi kuepuka faika/kifungo
TUMIA MIFUKO MBADALA, TUNZA MAZINGIRA.
IMETOLEWA NA
Mkurugenzi Mtendaji [H/W]
MASASI
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa