• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Uchaguzi

Dhumuni  la kuanzishwa kwa kitengo hiki ni kuhakisha zoezi la uchaguzi wa viongozi mbalimbali kwenye Halmashauri wakiwemo Rais, Wabunge, Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji pamoja na wajumbe wa Halmshauri ya Vijiji linafanikiwa.kitengo hiki kwa kiasi kikubwa hufanya kazi kwa ukaribu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Kitengo cha Uchaguzi cha Mkoa.

Kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya  uchaguzi nchini ,Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri ndiye Msimamizi wa Uchaguzi kwenye majimbo yote yaliyoko kwenye halmashauri yake kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kwa mamlaka aliyopewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi  humteua Afisa ambaye hufanya shughuli zote zinazohusiana na Uchaguzi  kwenye Halmashauri kwa niaba ya Mkurugrenzi Mtendaji. Afisa huyo ndiye  Afisa Uchaguzi wa Halmashauri.

MAJUKUMU YA KITENGO CHA UCHAGUZI CHA HALMASHAURI.

  1. Kitengo kinashughulika na uratibu wa masuala yote yahusuyo uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye halmashauri yaani uchaguzi wa Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji pamoja na wajumbe wa Halmashauri za serikali za vijiji.
  2. Kitengo kinashughulika na uratibu wa masuala yote yahusuyo Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwenye halmashauri yaani uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.
  3. Kitengo kinashughulika na uhakiki wa vitongoji, vijiji, kata na majimbo ya uchaguzi yaliyopo kwenye Halmashauri.
  4. Kitengo kinashughulika na uandaaji wa bajeti na mipango ihusuyo uchaguzi kwenye Halmshauri.
  5. Kitengo kinafanya kazi nyingine zozote zinazohusiana na uchaguzi kwenye Halmashauri kwa kadri itakavyoelekezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri.

MAJIMBO YA UCHAGUZI.

Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ina jumla ya vitongoji 889,vijiji 166 na kata 34 ambazo ziko ndani ya  majimbo mawili ya Uchaguzi ya  halmshauri ambayo ni Jimbo la Lulindi ambalo lina ukubwa wa sqkm 1961.4 na jimbo la Ndanda ambalo linaukubwa wa sqkm 1868.5.

 

MIONGOZO ,KANUNI NA SHERIA ZINAZOSIMAMIA UCHAGUZI NCHINI.

Kitengo kinapata nguvu ya kufanya uratibu kwenye  masuala yote yahusuyo uchaguzi kwani nchi imejiwekea  miongozo, kanuni na sheria mbalimbali zinazotoa mamlaka kwa vyombo vinavyohusika na uchaguzi kutekeleza majukumu yake ambazo ni -

  1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  2. Sheria ya Taifa ya  Uchaguzi (iliyofanyiwa mapitio 2015).
  3. Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015.
  4. Sheria ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa (iliyofanyiwa mapitio 2015 ).  
  5. Kanuni za Serikali za mitaa za uchaguzi wa madiwani za mwaka 2015.
  6. Gharama za uchaguzi za mwaka 2010.
  7. Sheria za vyama vya siasa ya mwaka 1992.

TARATIBU ZA KUPATA VIONGOZI.

Njia pekee itumikayo kupata viongozi nchini ni njia ya kupiga kura na  kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Ibara ya 5) inatoa haki kwa kila raia wa Tanzania aliyetimiza miaka kumi na minane kupiga kura katika uchaguzi unaofanywa Tanzania na wananchi. Na haki hii itatumiwa kwa kufuata masharti ya ibara ndogo ya (2) pamoja na masharti mengineyo ya Katiba hii na ya sheria zingine zinazotumika nchini zinazohusu uchaguzi .

Bunge laweza kutunga sheria na kuweka masharti yanayoweza kuzuia raia asitumie haki ya kupiga kura kutokana na yoyote kati ya sababu zifuatazo, yaani raia huyo -

Kuwa na uraia wa nchi nyingine.

Kuwa na ugonjwa wa akili

Kutiwa hatiani kwa makosa Fulani ya jinai

Kushindwa kuthibitisha au kutoa kitambulisho cha umri, uraia au uandikishwaji kama mpiga kura

Pia Bunge litatunga Sheria ya Uchaguzi na kuweka masharti kuhusu mambo yafuatayo –

  1. Kuanzisha Daftari la kudumu la wapiga kura na kuweka utaratibu wa kurekebisha yaliyomo katika Daftari hilo.
  2. Kutaja sehemu na nyakati za kuandikisha wapiga kura na kupiga kura.
  3. Utaratibu wa kumwezesha mpiga kura aliyejiandikisha sehemu moja kupiga kura sehemu nyingine na kutaja masharti ya utekelezaji wa utaratibu huo.
  4. Kutaja kazi na shughuli za Tume ya Uchaguzi na utaratibu wa kila uchaguzi ambao utaendeshwa chini ya uongozi na usimamizi wa Tume ya Uchaguzi.

UCHAGUZI WA RAIS NA WABUNGE .

Kwa mujibu wa katiba ibara ya 38 ,Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa katiba na sheria itakayoweka masharti kuhusu uchaguzi wa Rais ambayo itatungwa na Bunge kwa kufuata masharti ya Katiba.

Kitengo cha Uchaguzi kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi kwenye halmashauri ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji kimepatiwa  mamlaka ya kusimamia  zoezi la uchaguzi na kubandika matokeo ya uchaguzi ya urais lakini hakina mamlaka ya kutangaza kwani mwenye mamlaka ya Kutangaza matokea ya Uchaguzi wa Rais ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

SIFA ZA MTU KUCHAGULIWA KUWA RAIS ( IBARA YA 39).

Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri wa Muungano isipokuwa tu kama-

Ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia.

Ametimiza umri wa miaka arobaini

Ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa.

Anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

SIFA ZA MTU KUCHAGULIWA KUWA  MBUNGE  (IBARA YA 66 NA 67).

Mbunge ni mwakilishi wa wananchi katika Jimbo na mtu yeyote atachaguliwa kuwa mbunge ikiwa atakidhi sifa zifuatazo –

Ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja na ambaye anajua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili au kiingereza.

Ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa

Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

Msimamizi wa Uchaguzi kwenye halmashauri kupitia kitengo cha Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji amepatiwa  mamlaka ya kusimamia  zoezi la uchaguzi , kubandika na kutangaza matokeo ya uchaguzi ya Wabunge wa majimbo yaliyopo kwenye halmashauri yaani Jimbo la Lulindi na Jimbo la Ndanda.

UCHAGUZI WA MADIWANI 

Diwani ni mwakilishi wa wananchi kwenye kata na pia ndiye mjumbe wa kamati ya maendeleo ya kata.Diwani hupatikana kwa kuchaguliwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano. Msimamizi wa Uchaguzi kwenye halmashauri kupitia kitengo cha Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji amepatiwa  mamlaka ya kusimamia  zoezi la uchaguzi , kubandika na kutangaza matokeo ya uchaguzi ya Madiwani waliochaguliwa kwenye kata  34 za Halmshauri za Wilaya ya Masasi.

SIFA ZA KUGOMBEA UDIWANI

Mtu yeyote anaweza kugombea na kuchaguliwa kuwa Diwani iwapo anakidhi sifa  zifuatazo –

Awe ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Awe ametimiza umri wa miaka ishirini na moja au zaidi

Awe na akili timamu

Awe ni mkazi wa kata husika

Anaweza kusoma na kuandika Kiswahili na kiingereza

Awe ni mwanachamawa wa chama cha siasa kilichosajiliwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, sura ya 25 na chama chake kimemteua akiwakilishe kwenye uchaguzi husika.

Awe na njia halali za kujipatia kipato

Asiwe amehukumiwa kwa kosa la ukwepaji kodi ndani ya  kipindi cha miaka mitano kabla ya uchaguzi

Asiwe amehukumiwa kifo au amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita jela.

VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA

Katika vijiji nafasi zinazogombewa ni Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji, wajumbe wa halmashauri ya kijiji na wajumbe wa viti maalumu wanawake, na kati wajumbe watakao chaguliwa  idadi ya wanawake itakuwa nusu au zaidi ya wajumbe wote. Idadi ya wajumbe wa kijiji haitazidi ishirini na tano.na kwa kiasi kikubwa Tume ya Uchaguzi huwa haijihusishi na uchaguzi huu na badala yake TAMISEMI humpa mamlaka Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.

SIFA ZA WAGOMBEA

Mgombea kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa, vijiji na vitongozi anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo –

  1. Awe raia wa Tanzania na mkazi wa kawaida wa eneo husika.
  2. Mtu yeyote mwenye umri wa  kuanzia miaka 21 na kuendelea.
  3. Awe anajua kusoma na kuandika kiswahilina kiingereza.
  4. Mwenye kipato halali.
  5. Mwanachama na amedhaminiwa na chama cha siasa.
  6. Hajapatikana na hatia na kupata adhabu ya kifungo cha miezi sita.
  7. Asiye na ugonjwa wa akili.

WAJIBU WA VIONGOZI KWENYE MAJIMBO, KATA ,VIJIJI NA VITONGOJI

Kila kiongozi atakaechaguliwa  na wananchi  kupitia uchaguzi anawajibu wa -

  1. Kuangalia na kutambua shida za wananchi.
  2. Kuwaheshimu wananchi kwa kushirikiana katika kazi mbalimbali za kujenga nchi.
  3. Kushirikiana na viongozi wa sehemu yake ,Wilaya na Mkoa.
  4. Kuisadia serikali itawale vizuri
  5. Kuhudhuria vikao vyote vya kisheria .

CHANGAMOTO ZINAZO KABILI KITENGO CHA UCHAGUZI CHA HALMASHAURI

Kama ilivyoada changamoto huwa hazikosi kwenye kila jamboila kwa ufupi kitengo kinakabiliwa na changamoto kuu mbili –

  1. Kutishia kujihudhuru kwa wenyeviti wa vijji na wajumbe – hii nayo ni changamoto  ingawa sio sana hali hii husababishwa na migogoro lakini pia suala la kukosa posho za kujikimu kutokana na majukumu yao, ila  busara hutumika na kutatua migogoro hiyo na hatimaye viongozi hawa hujirudi na kuendelea na majukumu yao pia kwenye suala la posho kwa sasa serikali imesikia kilio cha na kwa kuanza sasa wenyevitiwa vijiji wameanza kupatiwa posho.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA III (JAN -MACHI 2025) INAYOTEKELEZWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI.

    May 06, 2025
  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA NeST NA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI

    March 12, 2025
  • KAMATI YA SIASA YA CCM WILAYA YA MASASI YAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI.

    March 06, 2025
  • MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YANATOA FURSA KILA MMOJA KUJUA HAKI YAKE YA MSINGI: MHE MAJALIWA

    March 06, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa