Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan leo tarehe 24 Septemba 2025 ameendelea na mikutano yake ya kampeni Mkoani Mtwara, ambapo akiwa katika Jimbo la Ndanda lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, amewahakikishia Wananchi kuwa Serikali itaendelea na juhudi za kuboresha na kuimarisha huduma za kijamii hususani katika sekta ya Afya, elimu na maji ili Wananchi wapate huduma hizo kwa karibu.
Amesema Serikali itaendelea kusimamia utoaji wa huduma muhimu za kijamii kwa Wananch wote "Kama kuna maeneo hayajapata maji tuwahakikishie maji yatapatikana, maeneo ambayo umeme haujafika wakandarasi wapo kazini na kazi inaendelea hivyo itabaki wewe mwenyewe (mwananchi) kuuza korosho na kuvuta umeme nyumani".
Aidha ameongeza kuwa maeneo ambayo vituo vya Afya havipo Serikali itaendelea kujenga na kukamilisha maboma yote ya Zahanati pamoja na vituo vya Afya ili kuhakikisha Wananchi wanapata huduma karibu na makazi yao.
Pia katika Sekta ya Elimu amesema kwamba Serikali itaendelea na sera yake ya elimu bure bila malipo na kuimarisha elimu Jumuishi kwa Watoto wenye mahitaji maalumu ili waweze kupata elimu .
Katika eneo la Ndanda ameitaja shule maalumu ya Lukuledi ambapo amesema" natambua hapa Ndanda kule Lukuledi kuna shule yenye watoto wenye mahitaji maalumu, lakini inashida kidogo nimeambiwa haina uzio, gari la usafiri na karakana ya mafunzo kwa vitendo ili kuboresha mazingira ya ujifunzaji kwaiyo niwahaidi vyote hivyo tutavikamilisha".alisema Samia.
Aidha akizungumzia suala la maji mhe.Dk.Samia Suluhu Hassan amewaeleza Wananchi kuwa kwasasa tayari Serikali imetoa fedha kiasi cha Shilingi Milioni 360 kwa ajili ya ujenzi wa machujio ya maji katika eneo la mradi wa Mwena- Liloya ili kuhakikisha Wananchi wanapata maji safi na salama mwaka mzima.
"Miaka mitano iliyopita tulijitahidi Serikali ilitoa fedha shilingi bilioni 13 tukatekeleza miradi 64 hapa, lakini bado miradi mingine inaendelea, lakini natambua katika Miradi ile tatizo letu kubwa maji yanakuwa ni machafu hivyo Serikali imeanza ujenzi wa machujio mawili ya maji, ikiwemo mradi wa Mwena- Liloya na pia tumeshamaliza usanifu na utafiti katika eneo la Ndanda na Nanganga ".
Hata hivyo amesisitiza kuwa huduma hizo za kijamii ni wajibu wa kawaida wa Serikali kwa Wananchi wake, na kwa hiyo haziwezi kuhesabiwa kama kazi ya Maendeleo bali ni haki ya msingi ya kila Mtanzania.
Kwa upande wake Mgombea Ubunge Jimbo la Ndanda kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Ndg.Faraji Buriani Nandala amesema kuwa tangu Serikali ya awamu ya sita iingie madarajani imepandisha sana thamani ya zao la korosho kwa kuwapatia pembejeo bure, hali ambayo imeongeza uzalishaji na kuleta tija kwa Wakulima sanjari na uwepo wa mfumo wa uuzaji wa korosho wa stakabadhi ghalani umesaidia wakulima kupata stahiki zao kwa wakati.
#Kazi na Utu tunasonga mbele#..
24 Septemba 2025.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa