• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Afya na Ustawi wa Jamii

IDARA YA AFYA, USTAWI WA JAMII NA LISHE

 

1.0 Utangulizi

Idara ya Afya Ustawi wa Jamii na Lishe ni moja ya idara 13 zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.Malengo makuu muhimu ya idara ni kutoa huduma za afya na tiba pamoja na huduma za ustawi wa jamii kwa  wana Masasi. Idara ina jumla ya watumishi 160 wa kada tofauti, hii ni sawa na asilimia 39.50 % ya jumla ya watumishi wote wanaohitajika ambao wamegawanyika katika kada ifuatavyo;- Daktari- 2, Katibu wa afya-1, Daktari Msaidizi-3,Mtaalam wa maabara 1,Mteknolojia maabara msaidizi 2, Afisa lishe 1,Afisa Ustawi wa Jamii-1, Afisa tabibu-14, Afisa tabibu msaidizi 17,Afisa afya 1,Afisa afya msaidizi 7,Afisa Muuguzi 2,Afisa muuguzi msaidizi 19,Wauguzi 37,Wahudumu wa afya 41,Wahudumu wa afya maabara 5, Fundi sanifu  msaidizi dawa-1,Fundi sanifu msaidizi maabara-3,Tabibi meno-1.

HUDUMA ZA TIBA                               

Halmashauri ina jumla ya vituo vya kutolea huduma 47, Huduma zitolewazo ni huduma za wagonjwa wa nje, Huduma za maabara, Huduma za matibabu na matunzo kwa watu wenye VVU, Huduma za ushauri Nasaha, Huduma za uchunguzi na vipimo, Huduma za mama na mtoto. Halmashauri ya wilaya ya Masasi ina Jumla ya vituo 47 vya kutolea huduma za afya. Mgawanyo wa vituo vituo hivyo umeambatanishwa:- Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ina Vituo 47 vya kutolea huduma za Afya zifuatavyo:-

JEDWALI 1:

HOSPITALI
VITUO VYA AFYA
ZAHANATI
Halmashauri
Binafsi
Dini
Serikali
Binafsi
Dini
Serikali
Binafsi
Dini
Taasisi za Serikali
0
0
1
2
0
2
31
1
9
1


Aidha orodha ya majina ya vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na umiliki wake ni kama ifuatavyo:-



S/NO
ID NO
JINA
AINA
UMILIKI
KITUO CHA AFYA/ ZAHANATI/ HOSPITALI YA WILAYA/ MKOA/ RUFAA/ TAIFA
KATA
KIJIJI/ MTAA
SERIKALI/ SHIRIKA/ TAASISI BINAFSI/ INAEDNESHWA KWA MAKUBALIANO ETC
1
93038
NAMATUTWE
ZAHANATI
NAMATUTWE
NAMATUTWE
SERIKALI
2
93069
NASINDI
ZAHANATI
CHIKUNJA
NASINDI
SERIKALI
3
93046
SHAURIMOYO                                                                                                                                                                                                                        
ZAHANATI
MPINDIMBI
SHAURIMOYO
SERIKALI
4
93005
CHIUNGUTWA
ZAHANATI
CHIUNGUTWA
CHIUNGUTWA
SERIKALI
5
93048
UTIMBE
ZAHANATI
LUPASO
UTIMBE
SERIKALI
6
93047
SINDANO
ZAHANATI
SINDANO
SINDANO
SERIKALI
7
93007
KANYIMBI
ZAHANATI
MPINDIMBI
KANYIMBI
SERIKALI
8
93006
CHIWALE
KITUO CHA AFYA
CHIWALE
CHIWALE
SERIKALI
9
93003
CHINGULUNGULU
ZAHANATI
NAMATUTWE
CHINGULUNGULU
SHIRIKA LA DINI
10
93001
CHIDYA
ZAHANATI
CHIWATA
CHIDYA
SERIKALI
11
93068
CHIKUNJA
ZAHANATI
CHIKUNJA
CHIKUNJA
SERIKALI
12
93070
MPETA
ZAHANATI
MPETA
MPETA
SERIKALI
13
93010
LUKULEDI
ZAHANATI
LUKULEDI
LUKULEDI 'A'
SHIRIKA LA DINI
14
93011
LULINDI
ZAHANATI
LULINDI
LULINDI
SERIKALI
15
93013
LUPASO
KITUO CHA AFYA
LUPASO
LUPASO
SHIRIKA LA DINI
16
93053
NAMOMBWE
ZAHANATI
MCHAURU
NAMOMBWE
SHIRIKA LA DINI
17
93015
MAKONG’ONDA
ZAHANATI
MAKONG'ONDA
MAKONG'ONDA
SERIKALI
18
93021
MBEMBA
ZAHANATI
CHIGUGU
MBEMBA
SERIKALI
19
93023
MBUYUNI
ZAHANATI
MBUYUNI
MBUYUNI
SERIKALI
20
93030
MCHAURU
ZAHANATI
MCHAURU
MCHAURU
SERIKALI
21
93026
MKULULU
ZAHANATI
MKULULU
MKULULU
SERIKALI
22
93058
MNAVIRA
ZAHANATI
MNAVIRA
MNAVIRA
SERIKALI
23
93033
MPINDIMBI
ZAHANATI
MPINDIMBI
MPINDIMBI
SERIKALI
24
93032
MIHIMA
ZAHANATI
MPANYANI
MIHIMA
SERIKALI
25
93055
MIJELEJELE
ZAHANATI
MIJELEJELE
MIJELEJELE
SERIKALI
26
93025
MITESA
ZAHANATI
MITESA
MITESA
SERIKALI
27
93035
NAGAGA
KITUO CHA AFYA
NAMALENGA
NAGAGA
SERIKALI
28
9345
NDANDA
HOSPITALI
NDANDA
MPOWORA
SHIRIKA LA DINI
29
93037
NAMAJANI
ZAHANATI
NAMAJANI
NAMAJANI
SERIKALI
30
93002
NAMBAYA
ZAHANATI
MLINGULA
NAMBAYA
SHIRIKA LA DINI
31
93044
NANJOTA
ZAHANATI
NANJOTA
NANJOTA
SHIRIKA LA DINI
32
93039
NANGANGA
ZAHANATI
NANGANGA
NANGANGA
SERIKALI
33
93043
NANYINDWA
ZAHANATI
CHIWALE
NANYINDWA
SERIKALI
34
93041
TULIZO
ZAHANATI
NANGOO
NANGOO
SHIRIKA LA DINI
35
93049
TUMAINI
ZAHANATI
MWENA
CHIKUNDI
SHIRIKA LA DINI
36
93066
MKUNDI AMANI
ZAHANATI
MKULULU
MKUNDI AMANI
SERIKALI
37
93054
NAMWANGA
ZAHANATI
MKUNDI
MKOLOPOLA
SERIKALI
38
93014
MAJEMBE
ZAHANATI
MKUNDI
MAJEMBE
SERIKALI
39
93065
CHIKOWETI
ZAHANATI
MLINGULA
CHIKOWETI
SERIKALI
40
93071
MAGEREZA
ZAHANATI
NAMAJANI
NAMAHINGA
TAASISI YA SERIKALI
41
9309
LUATALA
ZAHANATI
SINDANO
LUATALA
SHIRIKA LA DINI
42
KITUO KIPYA
MAPILI
ZAHANATI
CHIKOROPOLA
MAPILI
SERIKALI
43
KITUO KIPYA
CHIKOLOPOLA
ZAHANATI
CHOKOROPOLA
CHIKOROPOLA
SERIKALI
44
KITUO KIPYA
ST. MICHAEL
ZAHANATI
LULINDI
LULINDI
SHIRIKA LA DINI
45
KITUO KIPYA
NAMALEMBO
ZAHANATI
MSIKISI
NAMALEMBO
SERIKALI
46
KITUO KIPYA
MWENA
ZAHANATI
MWENA
MWENA
SERIKALI
47
KITUO KIPYA
KATIJI
ZAHANATI
NAMAJANI
NAMAJANI
BINAFSI

 

 

 

 

 

Huduma za Kinga

Katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi inatoa huduma muhimu za kinga katika vituo vya kutolea huduma za afya na ngazi ya jamii.Huduma za kinga zitolewazo ni huduma za chanjo,huduma za usafi wa mazingira, ufuatiliaji wa magonjwa yanayotolewa taarifa, huduma za lishe,huduma za kuwarudisha wagonjwa katika hali ya awali na huduma za ustawi wa jamii. Huduma za chanjo zinatolewa katika vituo 42 vya kutolea huduma za afya na pia huduma hizo zinapatikana  kupitia huduma za mkoba ambayo hutolewa katika maeneo 16.

Uhifadhi wa taka ngumu na taka maji ni muhimu sana katika suala zima la la kuzuia magonjwa ya mlipuko. Katika jamii. Asilimia kubwa ya taka ngumu katika ngazi ya vijiji zinahifadhiwa kwa njia ya vyoo, Halmashauri ina jumla ya  kaya 89,538 ,zenye vyoo vya muda 62,538, zenye vyoo bora 20,443, na kaya zisizo na vyoo 6,391.

Utoaji wa huduma za lishe unasaidia kujenga jamii yenye  kinga thabiti ambayo kwa kiasi kikubwa inazuia mwili kupatwa na magonjwa.Huduma za utoaji wa matone ya  Vitamini A na dawa za minyoo zinafanyika chini ya mwamvuli wa kitengo cha lishe.

Usafiri na mawasiliano

Idara ya Afya Ustawi wa Jamii na lishe ina jumla ya magari 3 na pikipiki…….,magari hayo yote matatu yanatembea. Pamoja na kuwa na magari hayo machache, Halmashauri haina magari ya kubebea wagonjwa, hali hii inapelekea kuwa na tatizo kubwa katika suala zima la rufaa ya wagonjwa.

VITENGO MBALIMBALI VILIVYOPO KATIKA IDARA YA AFYA USTAWI WA JAMII NA LISHE

 

  1. Kitengo cha lishe

Kama Afisa lishe katika halmashauri anawajibika na kuhakikisha kuwa watoto, Vijana,Wanawake na Wanaume katika jamii wana lishe bora inayowapelekea kuwa na afya bora kwa ajili ya uzalishaji wenye tija utakaochangia kukuza uchumi na maendeleo endelevu lengo hili pia itafanikiwa  kwa kufanya mambo yafuatayo;

  • Kufanya usimamizi elekezi na shirikishi katika vituo vya kutolea huduma za Afya kuhusu maswala ya lishe kama matibabu ya utapiamlo kwa watoto waliochini ya miaka mitano na utoaji wa nyongeza ya virutubishi (Vitamini .A na Madini chuma)
  • Kutoa elimu ya lishe katika jamii (utumiaji wa chumvi yenye madini joto)
  • Kupokea maelekezo yanayohusiana na maswala ya lishe kutoka ngazi ya mkoa pale yanapoletwa.
  • Kuchambua takwimu za lishe za mwezi, robo na mwaka.
  • Kutoa taarifa za mara kwa mara za hali ya lishe katika ngazi ya wilaya
  1.  Kitengo cha Ustawi wa Jamii 

Kusuluhisha migogoro mbambalimbali ya nayohusu

                  malezi  ya watoto

                  ndoa zenye migogoro

                  watu waliodhulumiwa

      kutelekezwa

Kusaidia watu wenye matatizo ya kiafya (wasio jiweza ) kuwapatia rufaa za kimatibabu katika hospitali ,vituo vya afya  zahanati mbalimbali za serikari

kuhakikisha wazee wenye umri wa miaka 60+ wanapata huduma za afya zilizo bora  kupitia  mfuko wa afya ya jamii (CHF),Kwa kuwapatia kadi

kusaidia watoto waliokinzana na sheria

kunda mabaraza ya wazee na watotokwa ngazi ya halmashauri ,kata na vijiji

kuunda kamati za watu wenye ulemavu na kamati za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

kubaini  na kuandaa orodha ya watu wenye mahitaji maalumu na kusaidia  kuwapatia misaada mbalimbali.

kushughulikia maswala ya kiunyanyasaji wa kijinsia wanaofanyiwa wanawake na watoto kwa kuwapatia msaada wa kisheria .

 

 

  1. Kitengo cha mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF). 

 

Usimamizi shirikishi kwa vituo 43 vinavyo huduma za afya vilivyoingia mkataba na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Kuingiza madai yaliyopokelewa kila mwezi kwenye mfumo wa kieletroniki kwa kila siku (E-Claims).

Kuwapatia watoa huduma fomu za madai ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwaajili ya kwenda kutoa huduma kwa wanachama.

Kushughulikia fomu za wanachama wapya wanaojiunga na wale waliopoteza kadi zao na wenye matatizo mbalimbali yanayohusu NHIF.

Kuwapatia kadi mpya zilizotengenezwa kwa wanachama walioomba kadi.

Kuwapatia elimu ya Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya kwa wanachama wapya na wanaokuja kila siku kuchukuwa fomu za kujiunga.

Kusikiliza na kutatua matatizo ya wanachama kila siku.

  1. Kitengo cha mfuko wa afya ya jamii (CHF)

Kitengo cha Mfuko wa Afya ya Jamii ni kitengo KIlichoanzishwa kwa sheria Na. 1 ya mwaka 2001, kikiwa na lengo la kutoa huduma bora kwa Wananchi wasio katika ajira rasmi na kupunguza mzigo wa gharama za matibabu kwao.

Mfuko wa Afya ya Jamii CHF unatoa huduma kwa watu 6 ( Mkuu wa Kaya 1 na Wategemezi 5) toka katika Kaya  moja kwa Mwaka 1 ambapo kila mkuu wa Kaya huchangia Shilingi 10,000/ .

Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mpaka Machi, 2018 ina jumla ya Kaya Hai (Zilizolipia huduma kwa Mwaka 1) 19,086  kati ya kaya  68,887  sawa na asilimia 27.71   Halmashauri ina jumla ya  wanufaika 99,358 kati ya  264,765 sawa na asilimia 37.53.

 

  1.  Kitengo cha Mfuko wa Afya ya Jamii

 

Usimamizi shirikishi kwa vituo 33 vya Serikali vinavyotoa huduma za afya kwa Kadi.

Kupokea taarifa za mwezi toka katika vituo 33 vya Afya vya Serikali kuzichambua na kuziwasilisha katika vikao vya Kisheria vya Halmashauri na Wilaya na Mkoa.

kuandaa na kufanya mikutano ya ushawishi kuhimiza jamii kujiunga na Mfuko wa CHF kwa kushirikana na Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji, Waganga wafawidhi wa Zahanati, Wadau wa Maendeleo na wananchi.

Kushughulikia  usajili wa wanachama wapya wanaojiunga na kuwapatia kadi na wale wenye matatizo mbalimbali yanayohusu CHF.

Kutoa elimu ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa wanachama wapya na jamii katika mikutano ya Hadhara.

Kusimamia mapato na matumizi yote katika mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

  1. Kitengo cha Afisa Afya
  • Kukagua na kufuatilia usafi wa mazingira katika: -
  • Nyumba za kuishi – uwepo wa vyoo na utupaji wa takataka ,Nyumba za biashara , Vyoo
  • Usafi, Watumishi waliokizi vigezo vya afya ,Taasisi kama vile Shule za Msingi na Sekondari ,Vyuo ,Ofisi mbalimbali ,Vituo vya huduma za Afya
  • Kufanya zoezi la usimamizi shiriki kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
  • Kukagua na kupitisha ramani za majengo
  • Ukaguzi wa viwanda vya kutengeneza vyakula kama vile viwanda vya maji, viwanda vya kusindika nafaka.
  • Kusimamia utekelezaji wa shughuli za kuzuia maambukizi katika vituo vya kutole huduma za afya.
  • Kusimamia na kudhibiti uchafuzi wa mazingira utokanao na shughuli za kibinadamu kama vile moshi utokanao na uchomaji moto ovyo.
  • Kuhamasisha jamii juu ya udhibiti wa wadudu wadhurifu na waenezao magonjwa.
  • Kufuatilia na kudhibiti magonjwa ya milipuko ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu
  • Kusimamia na kuhakikisha shighuli za ujenzi anafuata maelekezo ya mipango miji
  • Kufanya ukaguzi kwenye vyanzo vya maji
  • Kufuatilia afya za wafanya kazi katika maeneo ya kazi
  1. Kitengo cha Famasi

Kitengo cha Famasi ni kitengo kimoja kati ya vitengo vilivyopo katika Idara ya Afya, ni kitengo kinachojishughulisha na uagizaji, utunzaji, usambazaji na usimamizi wa mfumo wa ugawaji dawa, vifaa tiba vitendanishi na vifaa vya Hospitali.

Malengo

Kuhakikisha Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi vinapatikana wakati wote katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

Majukumu ya kitengo

  • Kuwasilisha taarifa na maombi (R&R) za vituo vyakutolea huduma za afya na R&R ngazi ya Halmashauri kwa wakati.
  • Kupokea na kutunza dawa,vifaa tiba na vitendanishi vinavyopokelewa ngazi ya Halmashauri.
  • Kusambazaa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
  • Kufanya usimamizi shirikishi na ukaguzi wa store za dawa za vituo vya kutolea huduma za afya ili kuhakikisha uwajibikaji kazi.
  • Kupokea maombi ya maduka ya dawa  muhimu na kufanya ukaguzi.

Ratiba ya utoaji wa majukumu ya kitengo

  • Kila mwezi kuanzia 1-5 kusambaza /kugawa dawa za miradi  msonge kwa vituo vinavyohusika.
  • August, Novemba, Januari na Mei tarehe 6-14 kuandaa na kuingiza kwenye mfumo R&R za mradi msonge ngazi ya Halmashauri.
  • August, Novemba, Januari na Mei tarehe 15-21 kuingiza R&R kwenye mfumo wa kuidhinisha maombi hayo kwenye mfumo.
  • August, Novemba , Januari na Mei tarehe 22-30 kuhakiki ubora wa taarifa ngazi ya vituo.
  • Baada ya mwezi mmoja toka tarehe ya kuwasilisha fomu za R&R kwenye mfumo  upokeaji wa shehena kutoka  MSD kwa shehena za mradi msonge.
  • Miezi iliyobaki kuanzia tarehe 6-30 ya kila mwezi ni kufanya ziara za usimamizi wa vituo vya kutolea huduma za Afya na DLDM kufanya ukaguzi na kuandaa taarifa muhimu za ukaguzi.
  1. Kitengo cha maabara
  • Kuendesha zoezi la uwamasishaji wa upatikanaji wa damu salama katika Shule za Sekondari, Jamii na katika madhehebu ya Dini
  • Kuhakikisha damu salama zinapatika katika vituo vya kutolea huduma wakati wote
  • kuhakikisha vitendanishi, vifaa, na vifaa tiba vinavyo hitajika vinapatikana muda wote
  • Kufanya usimamizi shirikishi katika vituo vya kutolea huduma za afya na kuwajengea uwezo watumishi wanao toa huduma za afya
  • Kufanya usimamizi shirikishi kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kufanya maoteo sahihi ya vitendanishi, vifaa tiba na vifaa
  • Kuhakikisha utoaji na upimaji wa vipimo vya maabara unafanyika kwa usahihi
  • Kuandaa na kutuma ripoti za kitengo cha maabara zinazo hitajika

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA III (JAN -MACHI 2025) INAYOTEKELEZWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI.

    May 06, 2025
  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA NeST NA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI

    March 12, 2025
  • KAMATI YA SIASA YA CCM WILAYA YA MASASI YAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI.

    March 06, 2025
  • MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YANATOA FURSA KILA MMOJA KUJUA HAKI YAKE YA MSINGI: MHE MAJALIWA

    March 06, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa