• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Nyuki

UFUGAJI  NYUKI

           Ni kitengo kinachohusika na  uendelezaji na uboreshaji wa mazao yatokanayo na nyuki  hapa nchini kama vile asali ,inta, masega, poleni..nk.Ufugaji wa nyuki kwa sasa ni nguzo ya kuinuia uchumi kuanzia ngazi ya mtu binafsi, vikundi, Jumuiya hadi Taifa. Kulingana na umhimu na faida itakanayo na ufugaji nyuki ufugaji wa kisasa unasistizwa.

TUNAJIHUSISHA NA;

  • kusimamia na kuhamasisha vikundi mbalilmbali,Familia, mtu binafsi na jamii kwa ujumla vinavyojihusicha na ufugaji wa nyuki katika ufugaji wa kisasa wenye tija na chachu kubwa katika kuboresha uchumi wa jamii, familia, na mtu binafsi.
  • Kuanzisha  manzuki mapya ndani ya misiti ya halmashauri ya wilya ya masasi.
  • Kusimamia ubora wa mazoa yapatikanayo na nyuki ndani ya halmashauri.
  • Kutafuta soko la mazao yatokanayo na nyuki ndani ya halmashauri
  • Kusaidia upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya ufugaji nyuki  kama vile Mizinga ya kisasa, Smooker, Vazi la kulinia asali, vifaa vya kuchujia asali.
  • Kupata takwimu za  mavuno yapatikanayo na ufugaji nyuki ndani ya hamshauri kila mwaka.
  • Kutatua changamoto mbalimbali zinazowakumba wafugaji nyuki mfano kuhama kwa Nyuki ndani ya mizinga, Changamoto za magonjwa au wadudu wanaoathiri nyuki.
  • Kufanya survey ya maeneo ya msitu mipya ndani ya halmshauri ili kuanzissha manzuki  mapya.
  •  Kutembelea vikundi mbalimbali vya ufugaji  vilivyopo na vitakavyoanzishwa na kufanya mijadala ya kujenga uwezo juu ya ufugaji nyuki.
  • Kutoa elimu juu ya namna ya kufanya ukaguzi wa mizinga mara kwa mara.

NYUKI.

         Kwa kawaida makundi ya nyuki huanza kutafuta sehemu salama na yenye chakula kwa wingi kuanzia mwezi wa kumi katika mwaka mpaka mwezi wa nne kwa mwaka unaofuata.Kipindi hiki huwa na makundi mengi yanayozunguka hapa na pale kutafuta nyumba ambayo itawafaa kwa ajili ya makazi yao na kwa ajili ya kuhifadhia chakula.

Hiki ndio huwa kipindi muafaka sana kwa wafugaji kuanza kutega mizinga ambayo imeshaandaliwa kwa ajili ya kufugia nyuki.

Kutokana na hilo, mfugaji anapaswa kuanza kuandaa sehemu ya kufugiua nyuki na mizinga yake mapema zaidi kabla ya msimu huo kufika ili asiweze kukosa makundi ya nyuki.Unashauriwa kuanza kuandaa mazingira ya kufugia nyuki na mizinga angalau mwezi mmoja kabla kwa kusafisha, kukarabati au kutengeneza kile unachokihitaji.

VIFAA VINAVYOPASWA KUANDALIWA.

Kabla ya kuanza kufuga nyuki kuna vifaa ambavyo mfugaji wanyukiu anapaswa kuanza kuviandaa mapema kabla ya msimu wa ufugaji wa nyuki kufika.Vifaa hivyo ni kama vifuatavyo:-

UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.

Eneo ambalo kuna wanyama wa aina mbalimbali ambao wanaweza kufanya uharibifu mbalimbali wa mizinga pindi ikiwa na nyuki na kusababisha uharibifu wa mizinga, kuua nyuki au hata mnyama mwenyewe kufa kutokana na kudungwa na nyuki.Hivyo ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki ni vyema ukafanyika.

 

DHAMIRA YA UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.

Mabanda hayo ya kufugia nyuki yanaweza kuwa ya udongo, tofali au ya miti pekee pande zote, milango pamoja na kuezekwa kwa nyasi.

Kuna sababu mbalimbali ambazo zinasababisha mfugaji nyuki kuweza kujenga mabanda ya kufugia nyuki, miongoni mwa sababu hizo ni:-

 

 

1. Kukinga mizinga na jua na mvua.

Hii ni sababu moja wapo ambayo inasababisha mfugaji wa nyuki kuamua kujenga mabanda ya kufugia nyuki, mzinga unapokuwa kwenye kivuli huusaidia mzinga kuweza kudumu kwa kipindi kirefu, pia kivuli husaidia nyuki kufanya kazi zao kwa juhudi.Iwapo mzinga utakuwa upo kwenye jua nyuki hutumia muda mwingi kupunguza joto la ndani ya mzinga badala kutumia muda huo kwa ajili ya kutafuta chakula.

Nyuki wanapoona jua ni kali zaidi na kusababisha joto kali ndani ya mzinga huamua kuhama katika mzinga huo na kwenda kutafuta makazi sehemu nyingine.Hivyo nio vyema mzinga ukakaa kwenye kivuli na sehemu isiyoweza kunyeshewa na mvua.

Pia mvua inaponyeshea mzinga husababisha mbao kuweza kuoza ndani ya muda mfupi, hivyo kwa kujengea banda la kufugia nyuki huweza kuukinga mzinga wako dhidi ya mvua ambayo inasababisha kuozesha mbao za mzinga wako.

2. Kukinga na wanyama waharibifu

Mabanda haya ya kufugia nyuki husaidia sana kwa wanyama waharibifu wa mizinga kushindwa kuifikia mizinga lakini pia husaidia sana kupunguza mashambulizi ya nyuki kwa viumbe wengine.Mizinga huwekwa ndani ya banda na banda kufungwa milango.

3. Ulinzi na ukaguaji

Ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki husaidia sana kuiweka mizinga yako sehemu salama dhidi ya wezi wa mizinga au asali lakini pia husaidia sana wakati wa uangalizi wa mzinga.Mizinga inapokuwa pamoja uangalizi wa mizinga hiyo huwa ni rahisi sana na pia huweza kusaidia kipindi cha uvunaji na uwekaji wa kumbukumbu za kila mara.

Pembeni ya banda hilo sehemu ambazo mizinga inawekwa huwekwa matundu maalumu ya kutoka na kuingia nyuki kwa ajili ya kujitafutia chakula chao.

MIZINGA YA KUFUGIA NYUKI.

Mizinga ya kufugia nyuki inapaswa kuandaliwa mapema kabla ya msimu wa kukamata makundi ya nyuki haujafika.Mizinga inayopaswa kuandaliwa ni kama ifuatayo:-

1. Mzinga wa kibiashara

Huu ni mzinga wa kisasa unaotumika kwa wafugaji wa nyuki hasa wale wanaotaka kuvuna asali kwa wingi kwa ajili ya kuuza.Mzinga huu huweza kuzalisha asali kwa wingi kadri misimu ya uvunaji inavyoongezeka mwaka hadi mwaka.

Mzinga huu una sehemu kuu tatu kama zifuatazo:-

a. Box la kuzalishia watoto wa nyuki

Ni box ambalo kwa kawaida huwa la kwanza kwa upande wa chini.box hili ndilo ambalo huwa na mlandfo wa nyuki kuingia na kutoka pindi wanapokwenda na kutoka kwenye utafutaji wa chakula.Box hili hutumika na malikia wa nyuki kwa kutagia mayai pamoja na kulelea watoto ambao husubiri kuanguliwa na kuwa nyuki kamili.

Pia box hili hutumika kwa ajili ya nyuki kuhifadhia chakula chao kwa ajili ya msimu wa kiangazi, msimu ambao huwa hauna maua yenye chakula cha nyuki cha kutosha,Hivyo mfugaji hapaswi kuvuna asali anayoikuta katika brood box, kwa kuvuna asali unayoikuta katika brood box husababisha kundi lako kuhama kwa kukosa chakula.

Kwa kawaida matumizi ya mzinga huu huanza kuvuna asali baada ya wastani wa misimu miwili mikubwa yaani sawa na miaka miwili.Na mara baada ya kipindi hicho kipita mfugaji huweza kuanza kuvuna kwa vipindi tofauti tofauti vya mwaka na kuendelea.

 

 

b.  Kitenga malikia

Hiki ni kifaa kama nyavu ambacho huwekwa kati ya brood box na super box, wavu huu huweza kumzuia malikia asiweze kupanda katika super box kwa lengo la kutaga mayai.matundu ya waya huu ni madogo kulingana na umbile la nyuki watenda kazi peke yao.Hivyo malikia na madume ya nyuki hayawezi kupanda kuelekea kwenye super box.

c. Box la kuhifadhia asali

Hili ni box ambalo huwekwa juu mara tu baada ya queen excluder.Box hili huwa ni maalumu kwa nyuki watenda kazi kuweza kuhifadhi asali yao kwa wingi.Asali inayokuwa katika box hili haiwezi kuchanganyika na watoto wa nyuki wala chavua kutokana na kuwapo kwa queen excluder chini yake.Asali inayotoka katika Box hili huwa nzuri na safi kutokana na kutochanganyika na masega ambayo yalitumika kwa kuangulia watoto wa nyuki.

Uvinaji wa asali katika mzinga huu, mfugaji anapaswa kutoa frame zilizopo katika super box ambazo asali yake tayari imeiva.Mara baada ya kutoa frame hizo mfugaji anapaswa kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kisasa iitwayo  Honey Centrifuge Machine.Mashine hii huweza kufyonza asali yote iliyopo katika sega na kubakiza sega likiwa halina asali.

Mara baada ya hapo mfugaji anapaswa kurudisha sega hilo kwenye mzinga likiwa na frame yake ili nyuki aweze kujaza asali tena.Hii inamsaidia sana nyuki kumpunguzia kazi ya kujenga sega jipya la Sali kila baada ya mvuno wa asali na hivyo kuongeza uzalishaji wa asali mara dufu.Tofauti tu ya aina ya mzinga huu ni kwamba huwezi kupata zao la nta.

2. Mzinga wa viunzi

Huu ni mzinga wa teknolojia ya kati kutoka kwenye mizinga ya kienyeji na kuelekea mizinga ya kisasa.Mzinga huu uhifadhi wake wa asali hautofautiani sana na uhifadhi wa asali katika mizinga ya kienyeji, isipokuwa katika mzinga huu masega hupangwa kwa kufuata utaratibu wa viunzi vilivyowekwa.nyuki huweka sega moja katika kila kiunzi kimoja cha mzinga huu.

Mzinga huu pia haujagawanywa kwa kutenganisha sehemu za kuhifadhia asali na sehemu ya malikia kuangulia watoto.Hivyo asali itokayo katika mzinga huu huweza kuchanyanyika na watoto iwapo mfugaji hatakuwa makini katika uvunaji wa asali hiyo.

Uvunaji wa mzinga huu, mfugaji anapaswa kukata sega lote lenye asali pekee na kulihifadhi katika chombo kisafi kwa jili ya kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kusasa au kwa kutumia njia za kitamaduni.

 

BAADHI YA VIFAA VYA KUVUNIA MAZAO YA NYUKI

  • FAIDA ZA UFUGAJI  NYUKI

     

    Hutumika kukatia masega ya asali

    KISU

    Hutumika kukinga mikona na miiba ya nyuki

    GLOVES

    Vazi hili hutumika kukinga mwili na miiba ya nyuki wakati wa kuvuna asali na kukagua mizinga


     

    B.BEE BLASH-Hiki ni kifaa kinachotumika  kuwaonda nyuki juu ya masega ya asali wakati wa Ulinaji wa asal

    • ASALI
  •  

    23. Kupungua kwa usikivu.

    22. Harufu mwilini.

    20. Uchovu mwilini.

    19. Saratani.

    18. Kupungua kwa uzito.

    17. Madhara ya ngozi.

    16. Kuumwa na wadudu (kwa washawasha) wenye sumu.

    15. Chunusi.

    14. Umri wa kuishi.

    13. Flu.

    12. Ukosefu wa nguvu za kiumbe.

    11. Kinga ya mwili.

    10. Shinikizo la damu.

    9. Ugonjwa wa moyo

    8. Mchafuko wa tumbo.

    7. Ugumba

    6. Helemu (Cholestral).

    5. Maumivu ya jino.

    4. Maambukizo kwenye kibofu cha mkojo.

    3. Ukungu wa miguu.

    2. Kukatika kwa nywele.

    1. Ugonjwa wa viungo/maumivu na uvimbe.

    MATUMIZZI YA ASALI

    MAGONJWA YANAYOTIBIWA KWA

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA III (JAN -MACHI 2025) INAYOTEKELEZWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI.

    May 06, 2025
  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA NeST NA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI

    March 12, 2025
  • KAMATI YA SIASA YA CCM WILAYA YA MASASI YAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI.

    March 06, 2025
  • MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YANATOA FURSA KILA MMOJA KUJUA HAKI YAKE YA MSINGI: MHE MAJALIWA

    March 06, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa