Idara ya Elimu ya Sekondari ni moja ya idara za Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Idara hii ilianzishwa mwaka 2009 baada ya Serikali kugatua usimamizi na uendeshaji wa shule za sekondari kutoka kwenye Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwenda na kusimamiwa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (Halmashauri za Wilaya/Miji/Manispaa/Majiji).
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ina Jumla ya shule za sekondari 27, kati ya hizo shule 26 ni za Serikali na shule 1 ni ya mtu binafsi. Kati ya shule za Serikali 26, shule 23 ni shule za kutwa na shule 3 ni shule za bweni ikiwa mojawapo ni shule ya kidato cha tano na sita. Jumla ya wanafunzi wa shule za sekondari za Serikali ni 7293 wakiwemo wavulana 3965 na wasichana 3,328 na shule ya binafsi ina jumla ya wanafunzi wavulana 501. Halmashauri ina jumla ya wanafunzi kwa shule zote za Serikali na binafsi 7794 wakiwemo wavulana 4466 na wasichana 3328.
2. DIRA NA MWELEKEO
2.1 DIRA, DHIMA NA MALENGO YA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA 2014
Msingi wa elimu na mafunzo utajikita katika kumjengea Mtanzania misingi bora ya malezi, maadili, ujuzi,umahiri na kumwezesha kujitegemea. Elimu ya kujitegemea itaendelea kuongoza utoaji wa elimu na mafunzo kwa kuzingatia mabadiliko yanayotokea katika jamii, kisiasa, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia.
2.1.1 DIRA
Kuwa na Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa.
2.1.2 DHIMA
Kuinua ubora wa elimu na mafunzo na kuweka mifumo na taratibu zitakazowezesha kupata idadi kubwa ya Watanzania walioelimika na wanaopenda kujielimisha zaidi ili waweze kuchangia katika kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa letu.
2.2 LENGO LA JUMLA LA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO
Kuwa na Watanzania walioelimika na wenye maarifa na ujuzi kuweza kuchangia kwa haraka katika maendeleo ya Taifa na kuhimili ushindani.
3. ELIMU YA SEKONDARI
3.1 MATAMKO YA SERA KUHUSU ELIMU YA SEKONDARI
3.1.1 SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 1995
Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ilifafanua kuwe Elimu ya Sekondari ina maana ya Programu (Mpango) kamili wa elimu inayotolewa kulingana na Mitaala ya Serikali na kupatikana kwa wanafunzi ambao watakuwa wamemaliza elimu ya msingi.
Nchini Tanzania elimu rasmi ya shule za Sekondari ina ngazi mbili. Ngazi ya kwanza ni elimu ya sekondari ya Ngazi ya Kawaida ya miaka minne, ambapo ngazi ya pili ni Programu ya Miaka miwili ya elimu ya Sekondari ya ngazi ya Juu. Ngazi ya kawaida huanzia kidato cha I na kuishia kidato cha 4, wakati Ngazi ya Juu ina kidato cha 5 mpaka cha 6
3.1.2 SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014
Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 imerekebisha muda wa elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali ili kuleta tija, ufanisi na matumizi bora ya rasilimali
TAMKO
3.1.2.1 Serikali itaweka utaratibu wa elimu ya awali kuwa ya lazima na kutolewa kwa watoto wenye umri kati ya miaka mitatu hadi mitano kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja.
3.1.2.2 Serikali itaweka utaratibu wa elimumsingi kuwa ya lazima kuanzia darasa la kwanza hadi kidato ha nne; na kutolewa kwa miaka kumi na umri wa kwanza darasa la kwanza kuwa kati ya miaka minne hadi sita kulingana na maendeleo na uwezo wa mtoto kumudu masomo katika ngazi husika.
3.1.2.3 Serikali itaweka utaratibu wa kuhakikisha muda wa kukamilisha elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali za elimu baada ya elimumsingi unalenga mwanafunzi kupata ujuzi stahiki kulingana na Mfumo wa Tuzo wa Taifa.
3.1.2.4 Serikali itahakikisha kuwa elimumsingi katika mfumo wa umma inatolewa bila ada.
4. LENGO LA IDARA
Kutoa nafasi ya upataji maarifa, ujuzi na kuelewa ili wanafunzi wajiunge na taasisi za ufundi na mafunzo ya kitaalamu ya elimu ya juu.
5. VITENGO VILIVYOPO KATIKA IDARA
Idara ya elimu ya sekondari ina jumla ya vitengo viwili (3) ambavyo hufanya shughuli zake kwa ushirikiano na kumsaidia mkuu wa idara ambaye ni msimamizi mkuu wa shughuli za idara katika kuleta matokeo tarajiwa. Vitengo vya idara ni pamoja na kitengo cha Taaluma kinachosimamiwa na Afisa Elimu Taaluma Wilaya, kitengo cha Vifaa na Takwimu kinachosimamiwa na Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Wilaya na kitengo cha ufundi kinachosimamiwa na Afisa Ufundi wa Wilaya na vyote vikiwa chini ya mkuu wa idara ambaye ni Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya.
5.1 MAJUKUMU YA VITENGO
5.1.1 MAJUKUMU YA AFISA ELIMU TAALUMA (W)
Kusimamia masuala yahusuyo maendeleo ya taaluma na michezo katika shule za sekondari wilayani.
5.1.2 MAJUKUMU YA AFISA ELIMU VIFAA NA TAKWIMU (W)
Kukusanya kuchambua na kuunganisha takwimu mbalimbali zinazohusu elimu ya sekondari.
5.1.3 MAJUKUMU YA AFISA ELIMU UFUNDI
Kusimamia upanuzi wa elimu ya sekondari kusimamia ujenzi wa majengo mapya katika shule za zamani au katika kuanzisha Shule mpya.
kwa maelezo zaidi bofya hapa
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa