Kiswahili
  • English
  • Kiswahili
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Elimu Msingi


1.0: UTANGULIZI.

Idara ya Elimu Msingi ni mojawapo kati ya Idara mbalimbali zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Idara hii ina vitengo vinne ambavyo vinaongozwa na Wakuu wa vitengo ambao wanamsaidia Afisa Elimu katika kutekeleza majukumu yake ya Idara ya kila siku. Vitengo hivyo ni Elimu ya watu wazima, Taaluma, Vifaa na Takwimu na Utamaduni.

Kazi na majukumu ya kila kitengo yamefafanuliwa vizuri katika taarifa hii sehemu ya vitengo vilivyopo kwenye Idara. Ikumbukwe kwamba Idara ya Elimu Msingi ni moja ya Idara kubwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, hivyo majukumu yake ni amtambuka ambayo yanagusa Idara nyingine kama vile, Afya, Maji, Maendeleo ya Jamii, Kilimo na Mazingira.

Idara inafanya shughuli zake kwa kufuata sheria, kanuni, miongozo na taratibu zilizowekwa na TAMISEMI na Serikali kuu kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata Elimu bora itakayowawezesha kufaulu mitihani yao na kumudu maisha yao ya kila siku katika Nyanja mbalimbali. Idara ina Watumishi ambao wanaweza kutimiza malengo   yaliyowekwa na Idara endapo watasimamiwa na kuwepo mazingira ya kufundishia ikiwemo miundombinu mfano, Vyumba vya Madarasa, Madawati, na Matundu ya Vyoo.

2.0: DIRA YA MWELEKEO.

Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imedhamiria kwamba kujenga uwezo wa kutoa huduma bora na mzuri kwa wakazi wake wote ifikapo mwaka 2015.

MWELEKEO: Halmashauri ya Wilaya ya Masasi inachukua jukumu la kuhakikisha kuwa Jamii yote inashiriki, wake kwa waume katika kupanga na kutekeleza mipango yao ya kiuchumi na kijamii ili kuinua kipato cha mwananchi ifikapo mwaka 2015.

3.0: MALENGO YA IDARA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA.

Katika utoaji wa huduma Idara imejiwekea malengo mbalimbali yatakayosaidia utoaji wa Elimu bora katika Shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.

Katika kutekeleza majukumu yake Idara inashirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu ambao ni viongozi wa Serikali za mita, Idara na Taasisi mbalimbali zisizo za Serikali, mashirika ya dini, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOS) CBOS na wahisani mbalimbali.

 

YAFUATAYO NI MALENGO YA IDARA.

  • Kuandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule na kuwa na darasa la awali katika kila shule.
  • Kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanajua kusoma, kuandika na kuhesabu
  • Kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoacha shule kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo mimba na utoro.
  • Kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la nne na darasa la saba katika mitihani yao.
  • Kuondoa matatizo ya madawati, vyumba vya madarasa, nyumba za Walimu na matundu ya vyoo
  • Kuanzishwa vituo vya MEMKWA katika shule mbalimbali ili kuwapatia Elimu watoto waliokosa Elimu katika Mfumo rasmi
  • Kufuatilia ufundishaji katika shule zote zilizopo katika halamashauri  ili kuona kama walimu:-
  • Wanajiandaa kabla ya kuingia darasani
  • Wanaingia darasani na wanafundisha
  • Wanatoa mazoezi ya kutosha kwa wanafunzi
  • Wanafanya tathimini ya ufundishaji
  • Kuwa na uongozi wa shule ulio imara wenye uwezo wa kusimamia ufundishaji, nidhamu, ya Walimu na Wanafunzi na unaoshirikiana na kamati ya shule na jamii kwa ujumla katika maswala yanayohusu shule kama vile. Vikao, mapato ya shule, miradi ya miundombinu na mipaka ya shule.
  •  Kutumia vituo vya walimu (Crusters) kwa ajili ya kufundisha mambo mabalimbali ya kielimu yakiwemo matumizi ya  mitaala, Elimu nje ya Mfumo rasmi, usimamizi wa miradi ya shule, matumizi ya fedha zinazopelekwa na Serikali kwa ajili ya uendeshaji wa shule na ufundishaji wa mada ngumu.
  •  Kukuza vipaji vya wanafunzi katika fani za utamaduni na michezo kwa kusimamia shughuli za utamaduni kama vile, ngoma, nyimbo, mashairi, ngonjera, maigizo na michezo mbalimbali inayofanyika katika shule zote.
  •  Kila shule kuwa na mradi wa Elimu ya kujitegemea ambao utaongeza mapato ya shule na uhifadhi wa mazingira.
  •  Kuwahudumia walimu na wananchi kwa usawa na kwa haraka wanapokuwa na mahitaji ya kuhudumiwa na Ofisi ya Elimu kama vile, uhamisho wa wanafunzi, ruhusa, ugonjwa na vifo, kujibu barua za walimu kwa haraka, kupitisha mihtasari ya matumizi ya fedha za shule, kusikiliza shida na matatizo ya walimu na kuwathamini.
  •  Kutoa motisha kwa Walimu na Shule zilizofanya vizuri katika taaluma, michezo, usafi na utunzaji wa mazingira.
  •  Kuwa eneo lisilopokea rushwa (Curruption Freezone) ambapo huduma itatolewa kwa haki bila upendeleo, kwa haraka na bila usumbufu.
  •  Kushirikiana na wadau wa kisekta kama vile, Idara ya Elimu Sekondari, Ukaguzi wa Shule, Tume ya Utumishi wa Walimu na Chama cha Walimu Tanzania katika kusimamia utoaji wa Elimu bora na huduma bora kwa Walimu.
  •  Kila mdau wa Elimu anapata taarifa za Idara ya Elimu bila vikwazo kwa usahihi na haraka zinapohitajika.

4.0: VITENGO VYA IDARA NA MAJUKUMU YAKE

Kama ilivyoelezwa katika utangulizi wa taarifa hii idara ina vitengo vinne (4) ambavyo ni. 

Elimu ya Watu Wazima ambayo ndani yake kuna vitengo vidogo vitano (5) ambavyo ni vielelezo, ufundi, kilimo, Sayansi kimu na Elimu Maalum.

Taaluma

Vifaa na takwimu

Utamaduni ambacho ndani yake kuna kitengo kidogo cha michezo.

Idara inafanya kazi zake chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.

ANGALIA MUUNDO WA IDARA

            MKURUGENZI MTENDAJI (W)
                               AFISA ELIMU MSINGI 

           

AFISA ELIMU YA WATU WAZIMA
SAYANSI KIMU
KILIMO
UFUNDI
ELIMU MAALUM
VIELELEZO
TAALUMA
VIFAA NA TAKWIMU
UTAMADUNI

WARATIBU VITUO VYA WALIMU


MICHEZO

WARATIBU ELIMU KATA





WALIMU WAKUU

WALIMU

MAJUKUMU YA KILA KITENGO KATIKA IDARA.

  • Kitengo cha Elimu ya Watu wazima
  • Majukumu ya kitengo cha Elimu ya watu wazima pamoja na vitengo vyake vidogo ambavyo ni Vielelezo. Ufundi, Sayansi kimu na Elimu Maalum yameambatishwa katika taarifa hii angalia kiambatanisho (Namba 1)
  • Kitengo cha Taaluma.
  • Majukumu ya kitengo cha Taaluma yameambatanishwa katika taarifa hii angalia kiambatisho (namba 2)
  • Kitengo cha Vifaa na Takwimu.
  • Majukumu ya kitengo cha Vifaa na Takwimu yameambatanishwa  ,angalia kiambatisho (Namba 3)
  • Kitengo cha Utamaduni.
  • Majukumu ya kitengo cha Utamaduni   na kitengo cha michezo yameambatanishwa katika taarifa hii, angalia kiambatisho (Namba 4)

5.0   MAJUKUMU YA IDARA KWA UJUMLA

Idara ya elimu msingi ina majukumu mengi ambayo yanasaidia katika utoaji wa elimu bora, kwa ujumla  malengo ya idara ni haya yafuatayo:-

  • Kusimamia utoaji wa Elimu katika shule za awali ,Msingi ,Elimu ya watu wazima na Elimu Maalum
  • Kuinua kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka na kufikia kiwango cha juu.
  • Kuboresha miundombinu katika shule kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu
  • Kuhakikisha kuwa vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinapatikana kwa lengo la kutoa Elimu iliyo bora.
  • Kuwa kiungo kati ya Idara nyingine ndani ya Halmashauri katika utoaji wa Elimu bora katika maswala ya Afya,Kilimo ,Maji, Mazingira,Ustawi wa maendeleo ya jamii
  • Kushirikiana na Idara nyingine zinazomhudumia mwalimu kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa mwalimu.

IDADI YA WATUMISHI

S/NA

JINA LA MTUMISHI

CHEO

NAMBA YA SIMU

1.
Elizabeth Mlaponi
Afisa Elimu Wilaya
0658 – 004926
0787-004926
2.
Sylvester Kayombo
Afisa Elimu kilimo
0787-036391
3.
Charles Millanzi
Afisa Elimu Vielelezo
0768-897201
0714-940136
4.
Ruth Tunzo
Afisa Elimu Vielelezo
0787-563214
5.
Eugen Ngaeje
Afisa Elimu Ufundi
0767-520909
6.
Anthony Luoga
Afisa Michezo
0788-436930
7.
Andrea Magani
Afisa Elimu Maalum
0786-179874
8.
Rehema Mpokwa
Afisa Elimu Sayansi kimu
0783-104586
9.
Rajabu Saidi
Afisa Elimu Taaluma
0784-810452
10.
Fatuma Mchia
Afisa Elimu Taaluma
0786-881886
11.
Tatu L.Kazibure
Afisa Elimu Vifaa na Takwimu
0784-496533
12.
Athanas Myogu
Afisa Utamaduni
0782-585608
0769-052261
13
Abdul Millanzi
Afisa Utamaduni
0715-878679
14.
Evelyna Maona
Karani Masjala
0653-887389
15.
Mustafa Malunda
Mwalimu
0719-285501
16.
Mariam Wadi
Mwalimu

17
Ally Nassoro
Mhudumu

18
Modesta Millanzi
Katibu Muhtasi
0688-347038

          

6. MIONGOZO NA SERA MBALIMBALI

Idara ya Elimu Msingi inatumia Sera na Miongozo mbalimbali katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku miongoni mwake ni pamoja na:-

  • Sera ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya   mwaka 2014, ambayo moja ya malengo yake ni pamoja na kuwa na idadi ya kutosha ya wananchi walioelimika katika Sayansi na Teknolojia na kukidhi mahitaji ya Maendeleo ya Taifa. Katika kufikia malengo hayo Sera inatamka haya katika vifungu vifuatavyo:-
  • 3:2:7 Serikali itaimarisha muundo wa utaratibu waufundishaji wa masomo ya hisabati, Sayansi na Teknolojia katika ngazi zote za Elimu na mafunzo.
  • 3:2:8 Serikali itahakikisha matumizi zaidi ya Sayansi na Teknolojia katika Utoaji wa Elimu na mafunzo klatika ngazi zote.

Kiambatisho Na.1

MAJUKUMU YA UONGOZI YA AFISA ELIMU WATU WAZIMA WILAYA

  • Msaidizi wa Afisa Elimu Wilaya /Halmashauri kuhusu Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi (EWW/ENMRA)
  • Mshauri mkuu wa Afisa Elimu Wilaya /Halmashauri kuhusu Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi (EWW/ENMRA) katika Wilaya.
  • Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi katika Wilaya/Halmashauri
  • Kuandaa bajeti ya mahitaji ya kitengo cha Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi (EWW/ENMRA) katika wilaya ikiwemo mishahara ya watumishi , posho za wawezeshaji /walimu wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.
  • Kubuni mipango ya kuendeleza taaluma ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi yanayoendeshwa katika wilaya.
  • Kuratibu mashindano ya kitaaluma ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi (EWW/ENMRA) yanayaoendeshwa katika Halmashauri.
  • Kuandaa mahitaji na ugawaji wa raslimali zihusuzo Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi (EWW/ENMRA)
  • Kukusanya kuchanganua na kutayarisha taarifa za Utekelezaji wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi (EWW/ENMRA) katika wilaya na kuziwasilisha katika ngazi zote.
  • Kuandaa mafunzo kwa watekelezaji wa Elimu ya Watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi (EWW/ENMRA) katika ngazi ya Wilaya.
  • Kuratibu Shuguli zote za Elimu ya watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi (EWW/ENMRA) zinazoendeshwa na Wizara,Taasisi,mashirika ya Umma na ya Watu binafsi katika Wilaya na kutoa taarifa.
  • Kuratibu utoaji wa Elimu masafa na ya ana kwa ana kwa kushirikiana na mkufunzi mkazi wa taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoa na waratibu wa vituo katika Sekondari na Vyuo.
  •  Kuratibu utoaji wa Elimu ya Sekondari katika vituo vya ufundi stadi na vya watu binafsi nje ya Mfumo rasmi
  • Kuraibu mipango ya kufuta ujinga wa kutojua  kusoma kuandika na kuhesabu inavyoendeshwa na shule za sekondari
  •  Kupokea taarifa zaukaguzi wa madarasa na shughuli mbalimbali za Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi (EWW/ENMRA) na kufuatilia utekelezaji wa maamuzi.
  • Ni kiungo cha upashanaji wa habari za mipango ya kielimu kati ya Kata, Taasisi, Mashirika ya Umma na watu binafsi katika Wilaya/Halmashauri
  • Kuendesha mikutano na warsha za kuhamasisha viongozi wa Wilaya, Kata, Vijiji wananchi kuhusu masuala ya Elimu kwa ujumla.
  • Kusimamia maadhimisho ya juma la Elimu ya Watu wazima na juma la Elimu kwa wote katika Wilaya.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopewa na Mkuu wake wa kazi.

 

 MAJUKUMU YA AFISA ELIMU VIELELEZO WA WILAYA 

  1. Kusimamia upatikanaji wa vielelezo katika utoaji wa Elimu ya Msingi, Sekondari, Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.
  2.  Mshauri wa Afisa Elimu wa Msingi, Sekondari, Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi kuhusu masuala ya vielelezo vya elimu katika Halmashauri.
  3.  Kuandaa na kutunza kumbukumbu zote muhimu kuhusu Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.
  4.  Kusimamia taaluma ya uandishi wa vitabu vya kiada, ziada, magazeti na nakala mbalimbali kwa ajili ya Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi katika Halmashauri
  5.  Kushirikiana na Afisa Elimu Taaluma wa Msingi na Sekondari kuandaa vielelezo mbalimbali vya kuboresha ufundishaji wa masomo ya elimu ya msingi sekondari Elimu ya watu wazima nje ya Mfumo rasmi.
  6.  Kushirikiana na Afisa Elimu Taaluma wa Msingi na Sekondari mhariri wa magazeti vijijini wa kanda katika kuandaa na kuendesha mafunzo kwa njia ya filamu, video, Tv, Mabango na vipeperushi.
  7. Kupokea, kuhifadhi na kusambaza vifaa vyote vya Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi katika Halmashauri
  8.  Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi

 

 

  MAJUKUMU YA AFISA  ELIMU UFUNDI WA WILAYA

  1. Mshauri wa Afisa Elimu wa msingi ,sekondari na Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi kuhusu masuala ya elimu ya ufundi katika Halmashauri
  2.  Kusimamia elimu ya ufundi katika shule za msingi na sekondari vituo vya elimu ya watu wazima na elimu nje ya Mfumo rasmi
  3.  Kuandaa makadirio ya matumizi ya fedha kwa ajili ya kutekeleza mipango ya ufundi katika shule za msingi na Sekondari na Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi ili yaingizwe katika bajeti ya Halmashauri
  4.  Kuratibu mipango yote ya elimu ya ufundi iliyoendeshwa na wizara taasisi mashirika ya umma ya kijamii na watu binafsi.
  5. Kuratibu uendeshaji wa miradi ya ufundi ya uzalishaji mali katika shule za sekondari vituo vya elimu ya watu wazimu nje ya Mfumo rasmi shule za ufundi stadi na msingi kwa kushirikiana na shirika la SIDO.
  6.  Kuhakikisha usalama kusimamia uendeshaji wa mitihani ya ufundi stadi katika Halmashauri.
  7.  Kuteua na kupanga walimu wa ufundi katika vituo vya shule kwa kushirikiana na Afisa Elimu Msingi na Sekondari.
  8.  Kushirikiana na Afisa Elimu vifaa na Takwimu Mratibu wa Elimu maalum na Mhandisi Wilaya kuhakikisha ujenzi wa madarasa nyumba za walimu na vyoo na majengo mengine ya shule yanajengwa kwa kufuata vipimo sahihi vinavyotolewa na Wizara na Elimu na mafunzo ya ufundi.
  9.  Kutayarisha taarifa ya utekelezaji wa elimu ufundi ya kila robo mwaka, nusu na mwaka mzima na kuziwasilisha katika sehemu zote zinzohusika.
  10.  Kusimamia ufunguzi wa vituo vya ufundi na sekondari kulingana na mwongozo wa Wizara.
  11.  Kushirikiana na Afisa Elimu Taaluma msingi na sekondari kuandaa na kuendesha mafunzo ya kujenga uwezo wa walimu wa ufundi katika ngazi ya Wilaya.
  12.  Kufuatilia taarifa za ukaguzi wa shughuli za ufundi katika shule za Msingi, sekondari na vituo vya Elimu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.
  13. Kupokea na kuweka takwimu sahihi za idadi ya wanafunzi walimu  na wafanyakazi wasio walimu wa shughuli za ufundi katika shule za msingi, Sekondari, vituo vya Elimu ya watu wazima na Elimu ya nje ya Mfumo rasmi.
  14.  Kuhamasisha wenye taaluma ya ufundi kujiunga na mafunzo ya elimu ya ufundi kwa lengo la kupata waalimu wataalamu

  MAJUKUMU YA AFISA ELIMU SAYANSI KIMU WA WILAYA.

Mshauri wa Afisa Elimu Msingi, sekondari na elimu ya watu wazima kuhusu masuala ya elimu ya sayansi kimu katika Halmashauri.

 Kuratibu shughuli zote za afya na lishe katika shule za msingi sekondari vituo vya elimu ya watu wazima na elimu nje ya Mfumo rasmi.

 Kushirikiana na Afisa Elimu Taaluma msingi na sekondari kutoa ushauri na kuandaa mafunzo kwa walimu wanaofundisha somo la sayansikimu na afya katika shule za msingi, sekondari , Elimu ya watu wazima na elimu ya nje ya Mfumo rasmi.

 Kutoa ushauri nasaha na unasihi kwa walimu, wazazi na wanafunzi kuhusu afya ya uzazi na malezi bora na tabia njema.

 Kuanzisha vituo vipya vya sayansi kimu na afya katika shule za msingi sekondari vituo vya elimu ya watu wazima na elimu nje ya Mfumo rasmi na kushauri namna ya kuviendesha kufuatana na mwongozo wa Wizara.

 Kuratibu na kusimamia uendeshaji wa miradi ya sayansi kimu na  uzalishaji mali katika shule za msingi, sekondari vituo vya watu wazima na elimu nje ya Mfumo rasmi kwa  kushirikiana na walengwa.

 Kupendekeza uteuzi wa wa walimu wa sayansi kimu na afya  kwa kushirikiana na Afisa Elimu msingi sekondari na wakuu wa vituo vya Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.

 Kutafuta na kusimamia usambazaji wa vifaa vyote vya sayansi kimu na kuvipeleka katika shule na vituo vya Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.

 Kutayarisha taarifa za utekelezaji wa Elimu ya sayansi kimu na afya ya kila robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima na kuziwasilisha katika sehemu zote zinazohusika.

 Kupokea na kuweka takwimu sahihi za idadi ya wanafunzi, walimu na wafanyakazi wasilo walimu wa shughuli za sayansikimu na afya katika shule za msingi, sekondari, vituo vya Elimu ya watu wazima na Elimu ya nje ya Mfumo rasmi.

 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi

         MAJUKUMU YA AFISA KILIMO NA UFUGAJI WA WILAYA

  1. Kusimamia Elimu ya kilimo na ufugaji katika shule sekondari, Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.
  2.  Mshauri wa Afisa Elimu Msingi, Sekondari, elimu ya watu wazima na Elimu ya nje ya Mfuno wa rasmi kuhusu masuala ya Elimu ya KIlimo na Ufugaji katika Halmashauri.
  3.  Kuandaa makadirio ya matumizi ya fedha kwa ajili ya kutekeleza mipango ya kilimo na ufugaji katika shule za msingi, sekondari na vituo vya elimu ya watu wazima na Elimu ya nje ya Mfuno wa rasmi ili yaingizwe katika mipango na bajeti za Halmashauri.
  4.  Kushirikiana na Afisa Kilimo na Ufugaji wa Halmashauri katika kuratibu nakusimamia shughuli zinazohusiana na kilimo na ufugaji katika shule za msingi sekondari na vituo vya Elimu ya watu wazima na Elimu ya nje ya Mfumo wa rasmi.
  5. Kufuatilia na kuhimiza uanzishaji wa vituo vipya vya kilimo na ufugaji kulingana na mwongozo wa Wizara.
  6. kushirikiana na maafisa Taaluma wa msingi ,sekondari na Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya mfumo rasmi katika kupanga na kuendesha semina, warsha na mafunzo kwa walimu wa kilimo na ufugaji katika shule za msingi,sekondari na vituo vya Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.
  7. kusimamia usalama,uendeshaji na usahihishaji wa mitihani ya kilimo na ufugaji katika shule za msingi ,Sekondari, Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi kwa kushirikiana na walengwa.
  8. kuratibu na kusimamia uendeshaji wa Miradi ya uzalishaji mali kama kilimo na ufugaji katika shule za msingi,Sekondari, Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.
  9.  kutafuta na kusimamia usambazaji wa vifaa vyote vya kilimo na ufugaji katika shule na vituo vya Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.
  10. kufanya uchambuzi yakinifu kuona kama muhtasari  na masomo ya kilimo na ufugaji inaoana na mazingira ya walengwa na kuwasilisha mapendekezo katika ngazi husika.
  11. kushirikiana na Afisa Ardhi wa Halmashauri ili kuhakikisha kwamba kila eneo la shule ya msingi na Sekondari linapimwa na kupata hati miliki.
  12. kutayarisha taarifa za utekelezaji wa Elimu ya kilimo na ufugaji ya  kila robo mwaka ,nusu na mwaka mzima na kuziwasilisha katika sehemu zote zinazohusika.
  13. kufuatilia taarifa za ukaguzi wa shughuli za kilimo na ufuatiliaji katika shule za msingi,sekondari na vituo vya elimu ya watu wazima na Elimu nje ya mfumo rasmi.
  14. Kupokea na kuweka  takwimu sahihi za idadi ya wanafunzi ,walimu na wafanyakazi wasio walimu wa shughuli za kilimo na ufugaji katika shule za msingi ,Sekondari na vituo vya Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi.
  15. kuhamasisha watu wenye Taaluma ya kilimo na ufugaji kujiunga na mafunzo ya Elimu ya kilimo na ufugaji kwa lengo la kupata walimu wataalamu.
  16. kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

MAJUKUMU YA KITENGO CHA ELIMU MAALUM

  1. kubainisha wanafunzi wenye ulemavu na mahitaji maalum na kuhifadhi kumbukumbu.
  2. Kubainisha walimu wenye ulemavu na kuhifadhi zao
  3. Kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji maalum na walemavu wanasajiliwa kufanya mtihani.
  4. Kusimamia na kuhakikisha  kuwa huduma kwa wanafunzi walemavu na wenye mahitaji maalum zinapatikana  kwa wakati.
  5. Kushirikiana na Afisa Elimu vifaa na Takwimu kupata takwimu sahihi za wanafunzi wenye ulemavu.
  6. Kuandaa na kutuma taarifa za kila robo za wanafunzi wenye mahitaji maalum na walemavu.
  7. kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

Kiambatisho Na.2

MAJUKUMU YA KITENGO CHA TAALUMA

  1.  Kuwa msaidizi wa Afisa Elimu Wilaya kuhusu:-

   Kufuatilia na kusimamia  utekelezaji wa taarifa za ukaguzi.

   Kubuni mipango ya kuinua kiwango cha taaluma katika Halmashauri nakusimamia utekelezaji wake.

   Kukusanya ,kuchanganua kutuma na kutoa takwimu sahihi

   Kubuni mipango ya kuimarisha na kuendeleza taaluma ya walimu na wanafunzi

   Kuratibu mashindano ya ya taaluma yanayoendeshwa katika wilaya

   Kuratibu utoaji wa huduma muhimu kwa walimu na wanafunzi kama vile uhamisho,mahudhurio na huduma za chakula.

  1. Kuratibu mafunzo ya walimu walio kazini
  2. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

 

 

 

 

 

 

 

Kiambatisho Na.3  

MAJUKUMU YA KITENGO CHA VIFAA NA TAKWIMU

  1. Kukusanya, kuchambua, kufafanua, kuhifadhi, kutoa  na kupokea takwimu za elimu ya msingi na kuziwasilisha zinakohitajika bila kuchelewa.
  2. Kufuatilia na kusimamia upanuzi na uimarishaji wa shule za msingi.
  3. Kufanya makisio ya idadi ya walimu kwa madaraja, kufuatana na upungufu na upanuzi.
  4. Kufanya makisio ya miundombinu na samani za shule zinazohitajika kulingana na idadi ya watumiaji.
  5. Kuratibu shughuli za Uagizaji na usambazaji wa vifaa vya shule kulingana na mahitaji ya shule na fungu la fedha.
  6. Kusimamia matumizi ya fedha kulingana na mahitaji, kwa kufuata kanuni na miongozo inayotolewa na Wizara.
  7. Kushirikiana na maafisa wengine kutoa huduma muhimu ikiwemo kusimamia mahudhurio ya walimu na wanafunzi, uhamisho na kuhamasisha jamii /shule kutoa   chakula cha mchana kwa wanafunzi.
  8. Kufanya makisio ya bajeti ya Idara kulingana na mahitaji kwa kuzingatia miongozo inayotolewa.
  9. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

Kiambatisho Na.4

 MAJUKUMU YA KITENGO CHA UTAMADUNI

  1. Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Sera ya Utamaduni ,Sera ya michezo na sera  ya mfuko wa Utamaduni katika ngazi ya wilaya.
  2. Kutoa ushauri juu ya uendeshaji wa utamaduni na michezo katika asasi mbalimbali katika ngazi ya wilaya.
  3. Kuratibu shughuli zote za maendeleo ya utamaduni na michezo katika wilaya.
  4. Kuwa msajili msaidizi wa vikundi vya sanaa ,vilabu vya michezo na vyama vya michezo katika wilaya.
  5. Kutoa ushauri nakufuatilia utekelezaji wa uhakika juu ya matumizi sahihi ya lugha ya Taifa (Kiswahili) katika wilaya.
  6. Kutambua na kuhifadhi maeneo mbalimbali ya kihistoria, makumbusho na nyaraka na matukio yanayojitokeza wilayani kwa ajili ya picha ,filamu na vitabu.
  7. Kutoa ushauri juu ya ujenzi na uendeshaji wa nadharia ya sanaa na majukwaa au kumbi zinazotumika kuonyeshea sanaa za maonyesho.
  8. Kufanya utafiti wa mila na desturi, fasihi simulizi ,sanaa za jadi na fani mbalimbali za michezo.
  9. Kushauri juu  ya mitaala ya mafunzo ya sanaa,Lugha,michezo na tafsiri katika shule na vyuo mbalimbali vinavyohusika.
  10. Kuandaa na kuendesha warsha na mafunzo mbalimbali kwa vikundi vya sanaa na vikundi vya michezo ili kuweza kuwajengea uwezo kiutendaji.
  11. Kusimamia uendeshaji wa vituo vya sanaa,lugha na majukumu ya sanaa za maonyesho.
  12. Kudhibiti uonyeshaji wote wa maonyesho mbalimbali ya sanaa yakiwemo filamu,cinema na uuzaji wa kanda za video ili kulinda maadili ya jamii ya Taifa kwa  jumla.
  13. Kuwa na utaratibu wa mahusiano wa sanaa na lugha kimataifa.
  14. Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu vipimo sahihi, uendeshaji na utunzaji wa viwanja vya michezo na maeneo ya burudani
  15. Kusimamia utekelezaji wa katiba na kanuni za vyama vya michezo katika wilaya.
  16. Kukusanya takwimu mbalimbali za utamaduni na michezo katika wilaya.
  17. TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULOI ZA ELIMU YA WATU WAZIMA-2018.pdf

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • WATENDAJI WA SERIKALI TEKELEZENI WAJIBU WENU WA KIKAZI,MSIJIHUSISHE NA MAMBO YA SIASA: BARAZA LA MADIWANI

    May 15, 2025
  • WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI NA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO ILI KUFANIKISHA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA AWAMU YA PILI.

    May 15, 2025
  • WATAALAMU MASASI DC WAPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA UJIBUJI HOJA ZA CAG.

    May 11, 2025
  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA III (JAN -MACHI 2025) INAYOTEKELEZWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI.

    May 06, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa