MRADI WA MAJI WA CHIPINGO -MKALIWATA
MRADI WA MAJI CHIPINGO - MKALIWATA umeanza kutekelezwa mwezi Machi mwaka 2014 na unatarajia kukamilika aprili 2019, Mradi una thamani ya shilingi bilioni 3.9 ambao umefadhiliwa na wizara ya maji na Umwagiliaji
Mradi ukikamilika unatarajia kuwanufaisha jumla ya wananchi 11,000 kutoka vijiji 11 ambavyo ni chipingo,mnavira,chikoropola,Namionyo,Mkaliwata,Manyuri,Mdue,Mapili, na Rahaleo wanaoishi katika Kata hizo ambao hawakuwa na huduma ya maji ya uhakika kwa muda mrefu.
katika mradi huu jumla ya vichotea maji 41 vinatarajiwa kujengwa katika vijiji 11 hivyo kufanya upatikanaji wa maji katika Halmashauri kuongezeka kutoka asilimia 51 utakuwa umeongezeka kwa asilimia 23 na hivyo kufanya Halmashauri kuwa na asilimia 74.1
kwa sasa mradi upo asilimia 80 ya utekelezaji ambapo shughuli za uchimbaji mtalo wa kulaza bomba, na ujenzi wa matanki ya kuhifadhia maji zimekamilika
Hili ni eneo lililojengwa chemba maalumu kwa ajili ya kuhifadhi maji,kuondoa taka pamoja na kuyachuja kabla ya matumizi
Hapa ni eneo la kwenye chanzo cha maji ndani ya mto Ruvuma
Hii ni chemba maalumu ya kupokelea maji na kuyahifadhi kutoka kwenye chanzo cha mto Ruvuma
Hiki ni kituo maalumu cha kuzalishia umeme unaotokana na nishati ya jua ambao una uwezo wa kuzalisha kilowats 32
Hili ni jengo maalumu kwa ajili ya ofisi pamoja na kuishi operata wa mradi
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa