Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara leo tarehe 03 Disemba 2025, limemchagua Diwani wa kata ya Ndanda (CCM ) mhe.Bashiru Fakih Mboneche kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, huku Diwani wa kata ya Chikundi mhe.Ismail Chilumba akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.

Katika mkutano huo Waheshimiwa Madiwani wote wameapishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Masasi mhe.Aisha Ndossy na baadaye wakafanya uchaguzi huo wa nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu Mwenyekiti ambapo jumla ya Madiwani 47 walipiga kura za ndio na hakuna kura yeyote iliyoharibika.

Akitangaza matokeo hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya Masasi Bi.Fatma Kubenea amesema "kwa matokeo haya na kwa mamlaka niliyonayo na mtangaza ndg.Bashiru Mboneche kuwa ndiye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi katika kipindi cha Miaka mitano ijayo".

Mkutano huo wa Baraza uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo uliopo Mbuyuni Masasi umeenda sambamba na kuundwa kwa Kamati za Kudumu za Halmashauri pamoja na uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati hizo, pamoja na Baraza kupokea Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji kuhuku kumbukumbu ya maamuzi ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri zilizofanyika kipindi ambacho Baraza lilivunjwa.


Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa