Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe.Rachel Kassanda amefungua rasmi mafunzo ya kuwajengea uwezo katika majukumu yao Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya mji na Wilaya ya Masasi, pamoja na Madiwani kutokea Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu yanayofanyika katika Ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi uliopo Masasi mjini.

Mafunzo hayo ya siku mbili kuanzia leo tarehe 30 hadi 31 Januari 2026, yanaendeshwa na Wakufunzi kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo Dodoma) yanahusisha mada mbalimbali zikiwemo Uongozi na Utawala Bora, Sheria za Uendeshaji wa shughuli za Serikali za Mitaa, Usimamizi wa ardhi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Usimamizi na udhibiti wa fedha za umma, uendeshaji wa Vikao na Mikutano katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Maadili ya Madiwani n.k

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mhe.Kassanda amewataka Waheshimiwa Madiwani kuyatumia mafunzo hayo kama nyenzo muhimu ya kuwaongezea uwelewa kuhusu majukumu yao ya kisheria, usimamizi wa rasilimali za umma pamoja na namna bora ya kushirikiana na wataalamu katika kusimamia Maendeleo mbalimbali kwa Wananchi.

Aidha, amewasisitiza madiwani umuhimu wa kuzingatia maslahi ya wananchi ambao wamewachagua kwa kuimarisha uwajibikaji, uwazi na nidhamu katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuharakisha Maendeleo ya Halmashauri na Wilaya zao kwa ujumla.
30/01/2026
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa