Imeelezwa kuwa Ujenzi wa Mabweni mawili ya Wasichana katika shule ya Sekondari ya Wasichana Ndwika iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara imepunguza mlundikano wa Wanafunzi mabwenini na hivyo kuongeza ari na motisha kwa Wanafunzi wa kike katika kujifunza.

Mradi pia umelenga kuboresha usalama, kupunguza utoro na kuimarisha ufaulu kwa kuwaweka karibu na shule.
Aidha ujenzi huu ni juhudi za serikali za kuhakikisha elimu bora na jumuishi kwa wote hasa kwa watoto wa kike.

Bi.Amina Bakari ni Mkuu wa shule ya Sekondari ya Wasichana Ndwika katika risala yake aliyoitoa jana tarehe 15 Januari 2026, mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Patrick Sawala alipowasili shuleni hapo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua hali ya Miundombinu ya Shule na uripoti wa wanafunzi mashuleni, ambapo amesema shule hiyo ni ya kidato cha tano na sita ni kongwe na miundombinu yake mingi ya zamani hivyo uwepo wa mabweni hayo yamesaidia kuwaondoa Wanafunzi kutumia miundo mbinu hatarishi zaidi kwa maisha yao.

Amesema tarehe 16 Oktoba 2024 shule hiyo ilipokea fedha kiasi cha Shilingi milioni 256 kwa ajili ya ujenzi wa Mabweni mawili kwa Wanafunzi 80 kupitia mradi wa SEQUIP ambao una lengo la kutanua wigo wa nafasi ya kupata elimu ya pili ya juu kwa Wanafunzi wa kike hapa nchini.
"Kwa hatua hii napenda kutoka shukrani kwa mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuekuboresha Mazingira ya kujifunza na kufundishia mashuleni katika Halmashauri yetu ya Wilaya ya Masasi "

Hata hivyo ifahamike kuwa mradi huu umekamilika tangu tarehe 31/03/2025 na kuanza kutumika mwezi julai 2025 mara baada ya kupokea wanafunzi wapya wa kidato cha tano kwa mwaka wa masomo 2025/2026

Shule ya Sekondari ya Wasichana Ndwika ina jumla ya Wanafunzi 696 kati ya hao kidato cha tano wapo 356 na kidato cha sita wapo 340.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa