Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ulioketi leo Disemba 03,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Mbuyuni Masasi, umempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg.Alphaxard Etanga na timu yake kwa kutekeleza kikamilifu shughuli zote za Maendeleo ambazo ziliachwa kipindi Baraza hilo lilipovunjwa.

Wamesema kupitia taarifa yake ya utendaji kazi wa Halmashauri kuhusu kumbukumbu ya maamuzi ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri zilizofanyika kipindi ambacho Baraza lilivunjwa, wameridhishwa na taarifa hiyo ya utekelezaji .

" Tunakupongeza sana Mkurugenzi wetu na timu yako, kwa kazi nzuri mliyoifanya huku nyuma kipindi sisi hatupo, mmeweka bidii katika kutekeleza masuala tuliyo waachia tu maamuzi, kwakweli mmefanya kazi kubwa mnastahili pongezi".

Miongoni mwa shughuli hizo zilizofanywa katika kipindi hicho cha mpito kupitia vikao vya kisheria vya kila mwezi vya Menejimenti ya Halmashauri,
maamuzi mbalimbali yalijadiliwa na kutekelezwa ikiwemo Ununuzi wa basi 1 (TATA) kwa gharama ya Shilingi milioni 155 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Halmashauri, Kuhusishwa kwa mkataba wa upangishaji wa Jengo la Ofisi ya Halmashauri baina ya Benki ya NMB na Halmashauri ambapo licha ya kuongeza Mapato ya ndani pia itasaidia kuongeza huduma za kibenki na kutanua huduma za kiuchumi n.k
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa