Ujenzi wa Jengo la madarasa 4 katika shule ya Msingi Nakachindu unaojengwa kwa msaada wa Serikali ya Japani kwa ushirikiano na shirika la TALIA
Shule za Msingi Nakachindu na Chipango zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara zilizokuwa na hali mbaya ya miundombinu ikiwemo madarasa na vyoo zitaondokana kabisa na upungufu wa miundombinu hiyo baada ya serikali ya Japani kupitia shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania life improvement association (TALIA) kujenga madarasa 7 na matundu ya vyoo 12 katika shule hizo kwa gharama ya shilingi milioni 182 065,100. shule ya Nakachindu inajengewa madarasa 4 yenye thamani ya silingi 96,991,150 na matundu ya vyoo 12 yenye gharama ya shilingi 11,561, 500 na shule ya Chipango madarasa 3 yenye thamani ya shilingi 74,512,450
mradi huo ulianza mwezi wa saba 2018 na utamalizika novemba 2018
Ujenzi wa Jengo la madarasa 3 katika shule ya Msingi Chipango unaojengwa kwa msaada wa Serikali ya Japani kwa ushirikiano na shirika la TALIA
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa