MRADI WA MAJI WA MWENA -LILOYA
MRADI WA MWENA -LILOYA umeanza kutekelezwa mwezi julai mwaka 2017 na unatarajia kukamilika aprili 2018 , Mradi una thamani ya shilingi bilioni 4.4
Mradi ukikamilika unatarajia kuwanufaisha jumla ya wananchi 66, 626 kutoka vijiji 18 wanaoishi katika Kata hizo ambao hawakuwa na huduma ya maji ya uhakika kwa muda mrefu.
katika mradi huu jumla ya vichotea maji 92 vinatarajiwa kujengwa katika vijiji 18 hivyo kufanya upatikanaji wa maji katika Halmashauri kuongezeka kutoka asilimia 51 hadi kufikia asilimia utakuwa umeongezeka kwa asilimia 23 na hivyo kufanya Halmashauri kuwa na asilimia 74.1
kwa sasa mradi upo asilimia 25 ya utekelezaji ambapo shughuli za uchimbaji mtalo wa kulaza bomba, ulaziji wa bomba na ujenzi wa matanki ya kuhifadhia maji zinaendelea.
Utandikaji wa mabomba katika mradi wa Maji MWENA -LILOYA
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa