MRADI WA UJENZI WA WODI YA AKINA MAMA NA WATOTO KATIKA KITUO CHA AFYA CHA CHIWALE.
UTANGULIZI
Mradi wa ujenzi wa wodi ya Akina Mama na Watoto katika Kituo cha Afya cha Chiwale ulianza rasimi mwezi Januari 2017 na unategemea kukamilika mwezi julai 2017.
GHARAMA ZA MRADI.
Mradi huu hadi kukamilika kwakwe utagharimu jumla Tsh. 108, 300,440.00 kati ya fedha hizo Tsh 80,000,000.00 zimetolewa na Serikali Kuu na Tsh 28,300,440.00 ni mchango wa Halamashauri. Hadi sasa jumla ya Tsh 30,120,139.00 zimeshatumika
MANUFAA YA MRADI
Mradi huu ukikamilika unatarajia kuwasaidia akina mama wajawazito wanaotarajia kujifungua, waliojifungua, na waliofanyiwa upasuaji.
Kituo cha Afya cha Chiwale kipo Kata ya Chiwale, Tarafa ya Lisekese katika mamlaka ya Halamashauri ya Wilaya ya Masasi. Kituo kinahudumia vijiji vitatu vya Chiwale, Ufukoni na Mkwapa pamoja na vijiji vya kata jirani.
Kituo cha afya chiwale kinahudumia watu 17,770, wanaume 7855 na wanawake 9915.
JENGO LA MRADI WA UJENZI WA WODI YA AKINA MAMA NA WATOTO KATIKA KITUO CHA AFYA CHA CHIWALE LIKIWA KWENYE HATUA YA KUEZEKWA
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa