Jumla ya Wenyeviti wa Vitongoji 886 kutoka kwenye Vijiji 166, Kata 34, tarafa 5 Halmashauri ya Wilaya Masasi Mkoani Mtwara wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo katika utendaji wa kazi.
Mafunzo hayo ambayo ni ya Siku mbili pekee yametolewa rasmi na Wawezeshaji kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa kilichopo jijini Dodoma ambapo Jana katika Siku ya Kwanza mafunzo yamewalenga Wenyeviti wa Vijiji 166 na kuhitimishwa leo hii tarehe 17/12/2024 huku nao walengwa wakuu wakiwa ni Wenyeviti wa vitongoji.
Akifungua mafunzo hayo leo Dec 17,2024 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Masasi Bi Beatrice Mwinuka ambaye ndiye mgeni rasmi Katika mafunzo hayo ya wenyeviti wa vitongoji amesema kwamba mafunzo hayo kwao ni muhimu Sana kwasababu wao tayari ni viongozi na Wananchi wanatambua kuwa wenyeviti hao wanajua kila kitu na Ndio maana Serikali imeona ipo haja yakuwaletea wawezeshaji ili wawapatie mafunzo elekezi ambayo yanaenda kuwa kielelezo kwa watu wanaowazunguka na kuwaamini kwa jambo lolote litakalotokea huko vitongojini basi wawe na majibu mazuri.
"Nimefurahi Sana kuonana na nyie, hongereni sana kwa ushindi , mlikuwa kwenye uchaguzi na mwisho wa siku mkaibuka washindi hivyo kilichonileta hapa ni kuja kuongea na nyinyi lakini pia kuwaeleza umuhimu wa mafunzo haya ambayo yanatolewa, tukihamasisha Jana kwa wenyeviti wa vijiji na leo tunamalizia Kwenu wenyeviti wa vitongoji maana katika utendaji kazi ni vizuri mkapewa maelekezo ya nini mnakwenda kukifanya, nini mnatakiwa kukisimamia na nini mnatakiwa kukitekeleza ili kusaidia kupunguza migogoro na kuhudumia Jamii kwa ujumla."
Mwinuka ameendelea kusema kuwa" Sisi ni viongozi katika vitongoji na tunaamini kwamba ukishachaguliwa kuwa kiongozi lazima wewe uwasimamie watu wako, ninachokiomba tuyaelewe haya mafunzo.
Bw. Enock Richard Halinga ni Mwenyekiti wa muda katika mafunzo hayo ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi hao waliopata mafunzo hayo kuwa waadilifu, kwasababu uadilifu unaanzia Nyumbani kwao, kwenye Jamii, kitongojini n.k , "naomba sana tuwe waadilifu nyakati zote na hasa katika heshima ya kuvaa vizuri Kama Watumishi wa umma kwasababu unaenda kuwatumikia Wananchi twendeni tukae waadilifu kuanzia mavazi,
na tabia ya kunywa pombe kupitiliza haitakiwi kwasababu wewe ni kiongozi Kuna mambo mengine yatatokea kwenye eneo lako nyakati za usiku utashindwa kuyatatua na wewe ndio kiongozi wetu ".
Dkt.Danford Sanga ni Mkurugenzi wa Taaluma- huduma saidizi ambaye ndiye wawezeshaji kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa Dodona amesema " leo tupo hapa Masasi kwaajili ya kuendesha mafunzo kwa wenyeviti wa vijiji/Mitaa/ Vitongoji ili kuwajengea uwezo wa uwajibikaji wawapo kazini, Sisi Chuo Cha Serikali za Mitaa ndio wenye jukumu kubwa la Serikali kwa ajili yakuwajengea uwezo huo".
*Kwaiyo tumetawanyika katika Halmashauri zote katika nchi hii , sio sisi tu bali Wataalamu wetu kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa wakishirikiana pamoja na Ofisi ya Rais kwenda kuwajengea uwezo viongozi wote walioshinda kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.,hili ndio Lengo kubwa la Sisi kuwepo.hapa."
Amesema zipo mada mbalimbali zaidi ya 9 zimefundishwa ikwemo sheria za Serikali za Mitaa, mafunzo juu ya utendaji wa wenyeviti wa Mitaa pamoja na ushirikiano kwa Watumishi, wadau, Watendaji wengine, Usimamizi wa Fedha, Usimamizi wa miradi n.k.
Bi.Amina Manyanga, Omari Muhere Pamoja na Christina Lucas ni miongoni mwa washiriki katika mafunzo hayo ambapo pamoja na kuiomba Serikali iangalie Namna bora ya kuwashika mikono wenyeviti wa vitongoji (Posho) ili kuipa thamani nafasi hiyo kwasababu zipo kazi nyingi hufanywa na wenyeviti wa vitongoji lakini hawalipwi chochote, pia wamewashukuru waaandaji wa mafunzo hayo Kwa Kutoa Elimu ya uwajibikaji, mawasiliano, nishamu , suala la utunzaji wa siri n.k ambapo wengi baadhi yao ni Wenyeviti wapya hivyo kupitia mafunzo haya yamewapa mwanga Kujua namna ya kuongoza kwa kufuata misingi ya sheria iliyowekwa,.
17/12/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa