Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mapema jana tarehe 04 Februari 2026 limefanya Mkutano wa Baraza la Madiwani Robo ya Pili huku likisisitiza kuongezwa juhudi katika ukusanyaji na udhibiti wa Mapato .

Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo uliopo Mbuyuni Masasi umelenga pia kupokea Taarifa za utekelezaji wa shughuli za Maendeleo za Halmashauri ngazi ya Kata, Kamati za kudumu za Halmashauri pamoja na TARURA, RUWASA NA NHIF.

Akiongoza Mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mhe.Bashiru Fakih Mboneche amesema ili kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi ambao ndio waliowapa dhamana hiyo, Waheshimiwa Madiwani wanatakiwa kuunganisha nguvu kwa pamoja na watumishi wa Halmashauri kwa kuzingatia Sheria na kanuni.
Amesema ushirikiano huo pia utaimarisha usimamizi wa mapato na matumizi ambayo yataleta matokeo chanya ya kiuchumi na Kijamii.

"Madiwani na watumishi mnapaswa kufanya kazi kama timu moja, kwasababu wote tunatoa huduma moja kwa umma, pia Madiwani mnatakiwa kushirikiana na Watendaji wa kata/ vijiji kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati,
na mkijenga Mazingira ya kuaminiana kwa amani kunaepusha upotevu wa muda na kuchochea maendeleo ya Halmashauri "

"Natoa rai, Madiwani sisi ndio Viongozi kwenye maeneo yetu, naomba tutenge muda kusimamia ipasavyo Miradi ya Maendeleo kwenye kata zetu, tumepewa dhamana, Uongozi tuliopewa kwenye kata zetu ninatamami wananchi tuwalipe mema kwa kusimamia yale maagizo yao, miradi ikija kwenye kata yako tenga muda nenda kaitembelee, isimamie, toa ushauri panapo bidi, msisubirie mpaka muda wa Baraza, naomba sana tufanye kazi kwa ushirikiano watumishi na Madiwani tuwe kitu kimoja ili Halmashauri iendelee kukua kwa ukusanyaji wa Mapato na ukamilishwaji wa miradi bora kwa wakati ..alisisitiza Mboneche
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Ndg.Optatus Lusolela ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu ameendelea kulithibitishia Baraza hilo kuwa Ofisi ya Mkurugenzi imeendelea kufanya vikao na Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali ili kuendelea kuweka mikakati madhubuti ya ukusanyaji na udhibiti wa mianya ya utoroshaji wa mapato sanjari na kuibua vyanzo vipya vya mapato"

Lusolela amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii ili kuwaletea Wananchi Maendeleo kupitia makusanyo hayo.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa