Waziri wa Ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mhe.Stergomena Lawrence Tax Leo Tarehe 13/11/2024 akihitimisha ziara yake Mkoani Mtwara ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa kituo Cha Mionzi (x-ray) kilichopo katika Kata ya Chiwale Halmashauri ya Wilaya Masasi Mkoani Mtwara.
Ziara hii ni muendelezo wa ziara ambazo alianza kuzifanya Tarehe 6/10/2024 Mkoani Mtwara, Lakini alilazimika kukatisha ziara baada ya kuwa amepewa majukumu mengine ya Kitaifa hivyo alilazimika kuondoka na kuhaidi atarudi tena.
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe hilo la msingi katika Jengo la Mionzi kwenye kituo Cha Afya Chiwale mhe.Tax amesema kwamba madhumuni ya ziara hiyo ni maagizo ya mhe.Rais Dokta Samia Suluhu Hassan ya kuwataka watembelee na kuangalia miradi iliyotekelezwa inaendeleaje na hatua gani imefikia, na Kama Kuna changamoto imesalia basi ziweze kutafutiwa ufumbuzi.
Amesema, mhe.Rais ana nia ya dhati ya kuhakikisha kwamba anawaletea Wananchi wake Maendeleo na anatatua changamoto zao, ha hii ameona katika miradi mbalimbali kwamba kuna fedha nyingi zimeletwa kwa kipindi cha uongozi wake tangu aingie madarakani.
"Mkoa wa Mtwara umekwisha pokea kiasi cha shilingi bilioni 740, Lakini kwa Masasi pekee imepokea kiasi cha shilingi bilioni 18.6 na hizo ndizo zimewezesha kutekeleza miradi mbalimbali ambayo nimeisikia katika sekta ya Afya, Elimu, Maji,barabara, umeme japo bado kuna changamoto Lakini si fedha hizi tu ambazo katika Jimbo hili la Ndanda, Wilaya hii imeendelea kunufaika na miradi mbalimbali kupitia katika fedha zinazopitia sekta nyinginezo".
Aidha, akizungumzia Jengo hilo la Mionzi mhe.Stergomena Tax ameendelea kuelezea kuwa kilichomleta hapo ni kuweka jiwe la msingi kituo Cha Mionzi" hii ni hatua kubwa sana kwasababu huduma zitakazotolewa katika kituo hiki ni za kisasa mno, ni huduma ambazo zinapatikana katika hospitali kubwa kubwa hivyo nimemuelewa vizuri mhe.mbunge Cecil Mwambe kwamba kituo hiki kwa ujumla wake ni kikubwa na kinaweza kupandishwa hadhi ya kuwa hospitali japo kuna baadhi ya changamoto ikwemo ukosefu wa wodi ya akina baba,hivyo nimelipokea na mimi nitayafikiaha kwa viongozi wangu wa juu".....alisema Waziri Tax
Hata hivyo mhe.Tax amehitimisha hotuba yake kwa kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kutenga fedha za mapato ya ndani na kuwezesha ujenzi huo wa kituo Cha Mionzi na hivyo amesisitiza kukamilisha haraka ujenzi huo ili wananchi wanufaike na mradi huo.
Hata hivyo ifahamike kuwa mradi unalenga Kutoa huduma ya Mionzi inayojumuisha huduma ya x-ray, ultrasound, mammography na kipimo Cha Moyo (ECG) hii inatokana na ongezeko la Wagonjwa wanaopata ajali, shida ya utumbo na uvimbe mbalimbali wa Ndani ya tumbo.
Aidha mradi huu utakapokamilika utahudumia Wananchi wapatao 50,163 wa Kata ya Chiwale na Kata jirani.
Mradi huu mpaka kukamilika kwake utagharimu kiasi cha shilingi 150,000,000.00 na Sasa tayari shilingi 130,000,000.00 zimetolewa Kutoka fedha za mapato ya ndani kwa awamu 3.
Pia mradi huu ambao kwasasa upo katika hatua ya umaliziaji unatekelezwa kwa mfumo wa force akaunti na ujenzi wake awamu ya Kwanza ulianza tarehe 19/04/2024 na kuisha tarehe 19/07/2024, awamu ya pili umeanza tarehe 13/09/2024 na unatarajia kukamilika Tarehe 13/12/2024
13/11/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa