Mkuu wa Wilaya ya Masasi mhe.lauter Kanoni amewakumbusha Wazazi/walezi ambao Watoto wao wamechaguliwa kuendelea na Elimu ya Sekondari 2025 kuacha matumizi ya fedha yasiyo na tija na badala yake wajenge tabia ya kufanya maandalizi mapema ili Watoto hao waweze kuripoti shuleni kwa wakati.
Mheshimiwa Kanoni ameyasema hayo Leo tarehe 05/11/2024 Katika mkutano wa baraza la Madiwani robo ya kwanza ambao umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri uliopo mbuyuni Masasi ambapo amesema kwamba" matokeo ya darasa la Saba yameshatoka, na madiwani wote mliopo hapa mnafahamu wanafunzi wanaotakiwa kwenda Sekondari kwenye Kata zenu, na mimi Vijana hawa mwaka huu kabla hawajaingia kwenye mitihani niliingia mkataba na Wazazi, na wale Wazazi walikiri kwamba watahakikisha Watoto wanakwenda Sekondari na mahitaji Yao watawatimizia, na mwisho wakaweka sahihi, hivyo naomba waheshimiwa Madiwani sasa hivi fedha watu wanazo mifukoni na hizo sherehe kwamba matumizi mengine hayana tija muwaelekeze hizo fedha wafanye maandalizi kwa wanafunzi wetu".
Aidha mhe.Kanoni ameongeza kuwa"Safari hii ile aibu tuliyopata mwaka huu ya Wanafunzi takribani 400 wanashindwa kwenda Sekondari hatutakuwa na msamaha tutashughulika na hao Wazazi,nendeni mkawaambie kwenye mikutano yenu suala la Elimu mimi Sina msamaha, naomba mniunge mkono kwa hili kwasababu wanafunzi wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza wanajulikana ni wale wenye ufaulu wa alama A,B.na C"...... alisisitiza mhe.Dc
Pia mhe.kanoni ameendelea kuelezea zaidi kuwa ili kuepuka changamoto zitakazojitokeza hapo baadaye amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuwatafuta Wazazi wote na Wanafunzi wao kwa kuwaandikia barua ya ukumbusho kuwa wanatakiwa kufanya maandalizi ya Watoto wao na ifikapo muda wa kuripoti shule basi wafanye hima.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa