Watoto wapatao 38,923 kati ya 37,272 katika halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wamepatiwa matone ya vitamin A ambapo idadi hiyo ni sawa asilimia 104.4 ya Watoto wote ambao wamepatiwa huduma hiyo.
Hayo yamebainishwa jana tarehe 14/08/2024 na Afisa lishe wa halmashauri ya wilaya ya Masasi Bi.Irene Shaban wakati alipokuwa akisoma taarifa ya utekelezaji wa Afua za lishe robo ya nne Januari -April kwenye kikao cha lishe kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo iliyopo Mbuyuni Masasi.
Amesema kuwa halmashauri ya Wilaya ya Masasi katika zoezi la mwezi wa afya na lishe kwa mtoto lililofanyika mwezi Januari 2024 limeonyesha kuwa watoto 38,923 kati ya watoto 37,272 walipatiwa matone ya vitamin A ambapo ni sawa na asilimia 104.4 ya watoto wote waliopatiwa huduma hiyo katika Halmashauri ya Wilaya Masasi.
"Matokeo haya yametokana na elimu ya afya na lishe inayofanywa na halmashauri kupitia Idara ya afya na kwamba hata jamii pia nayo imeanza kuwa na elimu ya kutosha zaidi kuhusu afya na lishe.
Bw.Muhsin Kombo ni mwakilishi kutoka divisheni ya Maendeleo ya jamii wa halmashauri hiyo naye amesema kuwa katika robo ya nne idara hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo sports development Aid imetoa mafunzo mbalimbali kwa Wanafunzi na wazazi/ walezi wa shule mbalimbali za sekondari ikiwemo shule ya Sekondari ya Namajani.
Amesema "elimu hii ya kuhimiza makundi katika jamii inazingatia zaidi lishe bora katika familia zao ambapo mfano tu Kuna yale mafunzo na elimu vilitolewa kupitia yale maadhimisho ya siku ya mtoto afrika mwaka huu 2024.
Amesema katika elimu hiyo jumla ya watu 105 wakiwemo wanaume 49 na wanawake 58 walifikiwa na kupatiwa elimu hiyo .
Naye Mganga mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt.Ruben Mwakilima ametumia nafasi hiyo Kutoa wito Kwa jamii kuwa na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara Ili kujua mwenendo mzima wa afya zao na pale mtu anapobainika kuwa na magonjwa basi hatua za kupatiwa matibabu zianze kufanyika.
15/08/2024
@.. Masasi DC
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa