Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Masasi Mkoani Mtwara Ndg.Ibrahim Chiputula ametoa agizo kwa kila kata kuhakikisha wanafanya mikutano ya Wazazi kwa kila Shule na kusisitizia suala la chakula mashuleni pamoja na kuwahimiza Wazazi juu ya umuhimu wa elimu kwa Watoto wao.
Chiputula ametoa agizo hilo leo julai 30/2024 katika kikao cha baraza la Madiwani robo ya nne kilichofanyika Katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri uliopo mbuyuni Masasi ambapo pamoja na mambo mengine mhe.chiputula amesema watu pekee wakuweza kusaidia kwenye suala la elimu ni watendaji wa kata na hasa wakijua wanachokifanya kwenye eneo lao kwa kuhakikisha jambo hilo linakwenda kisheria zaidi ili kuona Vijana wetu (Watoto) wanakwenda Shule.
Amesema kwa rekodi zetu"Halmashauri ya Wilaya ya Masasi hazipo vizuri na sote tunafahamu hakuna kitu kibaya kama unakwenda mkoani alafu unapatiwa zawadi ya kinyago (ikimaanisha hukufanya vizuri) hiyo hapana, haipendezi kwaiyo sasa mkakati tunaoweka tunakwenda kudhibiti hilo kwasababu kuna baadhi ya Wazazi wanakwepa majukumu yao na kutowajibika kuwapeleka watoto wao Shule."
Ameongeza kuwa pamoja na kazi kubwa inayofanywa na Idara ya Elimu Msingi marekebisho makubwa yaliyofanyika kumbadilisha walimu, kuondoa walimu, Lakini pia kuona mazingira bora kwa kushirikiana na wadhibiti ubora kufanya mabadiliko makubwa ili kuona tunapiga hatua huko tunakotarajia sisi kwa nafasi yetu Lakini Wazazi nao wanatuangusha kwenye maeneo hayo.
Agizo hilo linakuja baada ya uwepo wa taarifa inayoelezea kuwa Katika maeneo mengi ya Halmashauri hiyo hususani kwenye Kata ya Chikoropola, Namalenga, Namajani, Namatutwe, Chiwale, Mkalapa na Mkululu kwamba watoto wengi ambao walitakiwa waingie kidato cha kwanza mwaka huu 2024 mpaka sasa hawajaripoti Shule.
@Masasi DC
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa