Katika Picha inawaonyesha baadhi ya watekelezaji wa miradi mbalimbali ngazi ya vituo vya kutolea huduma (mashule na zahanati) pamoja na Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ambao tayari wamepokea fedha za mfuko wa Elimu na Mapato ya ndani wakipatiwa maelekezo ya namna nzuri ya kutekeleza miradi hiyo.
Miongoni mwa maelekezo hayo kwa mujibu wa mwongozo mpya wa manunuzi ni pamoja na kuzingatia taratibu zote za ununuzi na ugavi ambapo zinaelekeza utekelezaji wa mradi kwa force account (kwa kuunda Kamati mbili za miradi) , kuzingatia matumizi sahihi ya mfumo wa Usimamizi wa manunuzi ya umma NeST.
Maelekezo mengine ni namna bora ya kuwapata mafundi bora wenye vigezo, na kuzingatia vigezo vya kupata vifaa Bora vya ujenzi.
Pia uzingatiaji wa thamani ya fedha iliyotolewa na ubora wa kazi, sambamba na kuzingatia muda halisi wa kukamilika kwa miradi ambapo wametakiwa hadi ifikapo Jan 15, 2025 miradi hiyo yote Kila mmoja katika eneo lake iwe imekamilika na kukabidhiwa.
Zoezi hilo liimefanyikia Dec 17,2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo uliopo mbuyuni Masasi.
19/12/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa