Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Vijiji na Kata Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wapatao 220, leo tarehe 30/09/2024 wamepatiwa mafunzo maalum yanayolenga Kutoa mwongozo wa namna ya kusimamia Shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajia kufanyika Nov 27,2024.
Akifungua mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri hiyo uliopo Masasi mjini, Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya Masasi Bi.Beatrice Mwinuka amesema kwamba wamekutana hapo ili kupeana miongozo mbalimbali itakayo wawezesha kusimamia kwa uadilifu uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuchagua Viongozi katika maeneo yao kwa maana Mwenyekiti wa Kijiji, Kitongoji na wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji.
"Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa ndio dira ya Uchaguzi Mkuu wa hapo mwakani, hivyo kinachotakiwa ni kusimamia vizuri taratibu zote za Uchaguzi kwa kuzingatia 4R za mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwaiyo leo tunawapitisha kwenye mada mbalimbali ikiwemo Uandikishaji wapiga kura,Sifa za mpiga kura, Sifa za mgombea, uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa mgombea,kampeni uteuzi, rufani n.k ili mjue sasa nini ambacho kinatakiwa katika kusimamia" alisema Mwinuka.
Hata hivyo Mwinuka ameendelea kuwasisitiza washiriki hao kila mmoja kwa nafasi yake awajibike kwenye eneo lake ipasavyo kwa kuzingatia maelekezo na miongoni waliyopatiwa ili waweze kufanikisha zoezi hilo.
Mafunzo hayo pia yameenda sambamba na uapishwaji kwa washiriki hao ambapo wamekula kiapo Cha uaminifu na utunzaji Siri, pamoja na kiapo cha utii na uadilifu zoezi lililo ongozwa na Hakimu kutoka Mahakama ya Wilaya Masasi.
Kwa upande wake Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mtwara Bi.Edith Shayo pamoja na kuwashukuru washiriki hao kushiriki mafunzo hayo ambayo ndio kielelezo kwao katika usimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pia amesema Katika Mkoa wa Mtwara Halmashauri ya Wilaya Masasi inaongoza kwa ukubwa ukitofautisha na Halmashauri zingine zilizopo ndani ya Mkoa hivyo ni matumaini yake kupitia mafunzo hayo watazingatia kanuni na miongozo waliyopatiwa ili waweze kufanya vizuri katika usimamizi na Uchaguzi huo ufanyike vizuri na kuwa kielelezo katika maeneo mengine.
Uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa ambao unatarajia kufanyika Nov 27,2024 unaongozwa na kauli mbiu isemayo* Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, jitokeze kushiriki Uchaguzi "
30/09/2024
@.. Masasi DC
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa