Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa vituo vya kupigia kura 1,937 Jimbo la Ndanda na Lulindi wametakiwa kuzingatia kanuni, taratibu na miongozo yote itakayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi katika kipindi chote cha Uchaguzi Mkuu.

Hayo yamesemwa leo tarehe 26 Oktoba 2025 na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ndanda na Lulindi Ndg.Keneth Mgina wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa Wazimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa vituo vya kupigia kura yanayofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Masasi, Ukumbi wa Migongo Sisters pamoja na Ukumbi wa Migongo Brothers.

Amesema kwa kuzingatia viapo vyao itasaidia wao kutokuwa vyanzo vya malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa na kuwasihi kushirikiana na mawakala wa vyama vya siasa watakaokuwa vituoni kwa mujibu wa sheria.
"Dhamana mliyopewa ya kusimamia zoezi la kupiga kura na kuhesabu kura ni sehemu ya usimamizi na uratibu wa Uchaguzi wa Rais na wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara ni kubwa na nyeti na muhimu kwa mustakabali wa Taifa, hivyo kwa kutambua dhamana hii mliyopewa na Tume mtambue kuwa kwasasa mnategemewa sana kuzingatia Sheria, kanuni na maelekezo mtakayopewa hadi hapo tutakapokamilisha jukumu hili la uchaguzi mkuu,"......amesisitiza Mgina.

Mafunzo kwa Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa vituo vya kupigia kura Jimbo la Ndanda na Lulindi yanafanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia leo tarehe 26 - 27, Oktoba 2025 huku yakiwashirikisha washiriki 1937 ambao wameteuliwa kwa ajili ya kufanya kazi katika vituo 623 vya Uchaguzi katika Jimbo la Ndanda na Lulindi.

"Kura Yako Haki Yako Jitokeze kupiga kura
26/10/2025.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa