Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa vituo 1937 vya kupigia kura katika Jimbo la Ndanda na Lulindi , wameaswa kuzingatia maadili, uadilifu na uzalendo katika utekelezaji wa majukumu yao katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani ambao unatarajia kufanyika siku ya Jumatano tarehe 29 Oktoba 2025.
Akizugumza wakati akifunga mafunzo kwa Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa vituo vya kupigia kura Jimbo la Ndanda na Lulindi Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ndanda na Lulindi Ndg.Keneth Mgina amewataka wasimamizi na wasaidizi wa vituo vya kupigia kura ambao wamepata mafunzo hayo kuzingatia maelekezo yote waliyopewa ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa ufanisi na kwa kufuata taratibu zilizopo. .
Amesema jukumu walilopewa ni la kuaminika na linahitaji umakini, uwadilifu na utiifu kwa miongozo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, hivyo amewaasa washiriki hao kuwa mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa majukumu yao katika kipindi chote cha Uchaguzi Mkuu.
" Tume inawaagiza kupitia mafunzo mliyopewa tunahitaji mshirikiane na kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unafanyika kwa amani, utulivu na uwazi bila kuegemea chama chochote cha siasa.
"Jukumu la kusimamia uchaguzi ni dhamana kubwa na nyeti inayohitaji uadilifu, nidhamu na kufuata maelekezo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na mnapaswa kutoa kipaumbele kwa wapiga kura wenye mahitaji maalumu watakapofika kituoni, kusimamia kiapo cha kutunza siri, na kuhakikisha taarifa zote za uchaguzi zinatolewa kupitia ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi pekee. Aliongeza kuwa watumishi hao wanawajibika kwa Tume na si kwa mtu mwingine.'
Aidha, Mgina amewakumbusha Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wote kutambua kuwa katika kipindi chote cha uchaguzi hawapaswi kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa, na badala yake wajikite kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kwa kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi.
“Ndugu washiriki, dhamana mliyopewa ya kusimamia zoezi la upigaji na kuhesabu kura ni kubwa na nyeti kwa mustakabali wa Taifa letu. Ni wajibu wenu kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo mtakayopewa na INEC ili uchaguzi wa mwaka huu uwe wa amani na utulivu,” alisema Mgina.
Jumla ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa vituo vya kupigia kura wapatao 1937 kutoka
Jimbo la ndanda Na lulindi wanatarajia kusimamia Vituo vya kupigia kura 623 katika kata 34 za Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
"Kura Yako Haki Yako Jitokeze kupiga kura."
27/ 10/ 2025 .
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa