Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Selemani Mzee ameendesha Harambe ya kuichangia timu ya ndanda kama jitihada za kuisaidia timu hiyo kiuchumi ili iweze kuendelea na mashindano ya ligi kuu yanayoendelea
Harambe hiyo imejumuisha wadau wote wa michezo wakiwemo wafanyabiashara , wapenzi wa michezo, watumishi na wananchi wa kawaida kuichaingia timu hiyo ambapo kwa sasa haiko vizuri kimapato.
Akiongea katika Harambe hiyo jana, Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Selemani Mzee alisema kuwa kuwa “Timu ya ndanda ni timu tuliyoianzisha wenyewe na imekuwa na mafanikio makubwa, hivyo hatuna budi kuiwezesha ili iendelee kutuletea sifa katika wilaya yetu na mkoa kwa ujumla”
Uchangiaji utafanyika kwa kuchukua kitabu cha risiti chenye jumla ya risiti 50 na kiwango cha chini cha kuchangia ni shilingi 50,000. Masasi inatarajia kugawa vitabu 50 ambapo kila kitabu itatakiwa kukusanya kuanzia 500,000.
“Watu wa masasi nawakubali hatutashindwa kukusanya shilingi 25,0000,000 kwa vitabu 50 tunavyotarajia kuvigawa kwa wadau mbalimbali” alieleza Mkuu wa wilaya.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa