Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mhe.Kanali Patrick Sawala amesema, Mkoa wa Mtwara ni miongoni mwa mikoa iliyonufaika na matunda ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiwemo kuimarika kwa amani na utulivu ndani ya mkoa huo.
Matunda mengine ni kupiga hatua za kimaendeleo katika nyanja za kiuchumi, kijamii, na kisiasa, huku maendeleo haya yakitokana na mikakati mizuri iliyowekwa na Serikali kuanzia ngazi zote za uongozi iliopita hadi sasa kwani miradi mbalimbali ya maendeleo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa.
Amesema hayo Jana mapema April 26,2024 katika sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo kwa Wilaya ya Masasi yamefanyikia katika kijiji cha Nagaga kata ya Namalenga huku burudani mbalimbali kama vile kuvuta kamba, kukimbiza kuku,vikundi vya ngoma pamoja na nyimbo mbalimnali
zikiipamba sherehe hizo.
Amesema "sherehe za mwaka huu ni maalumu na zakipekee kwani Tanzania inatimiza miaka 60 ya Muungano wetu kwa maana hiyo kwa watu waliozaliwa tarehe 26 April 1964 siku ambayo Muungano ulikuwa unaasisiwa maana yake leo kama ni Watumishi wanakuwa wanastaafu utumishi wa umma."
Aidha, Mhe.Sawala ameendelea kwa kusema kuwa "hatua hii inaonyesha kwamba Muungamo wetu umedumu muda mrefu hivyo tunayo sababu ya kindugu na kijiografia kwa Wananchi wa pande zote mbili za Muungano tunaendelea kuwakumbuka Viongozi wetu walioasisi Muungano wakiongozwa na Hayati baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyererena Shekhe Abeid Aman Karume, Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani."
Ameongeza kuwa tunapoadhimisha miaka 60 ya Muungano, tuna kila sababu ya kujipongeza,kutafakari, kutathimi mafanikio ya mkoa wetu na kujikumbusha tulipotoka,tulipo sasa na tunapoelekea na huku tukirejea ule msisitizo wa mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan alipohutubia bunge la Jamhuri ya muungano w Tanzania tarehe 22 April 2021,alisisitiza kujenga nchi yetu kwa kuzingatia maridhiano, ustahimilivu, mabadiliko na kujenga upya nchi yetu hivyo msisitizo huu licha ya kutoa maono yakujenga nchi yetu unalenga pia kudumisha muungano,kuleta umoja bila kujali tofauti zetu za kisiasa,kidini na kikabila.
Hata hivyo ameendelea kuwaomba watanzania kuendelea kuisoma vizuri historia ya muungano na kujua asili yake, changamoto zake na namna zilivyotatuliwa ili kizazi cha sasa kiweze kuimarika .
Maadhimisho hayo kwa mwaka huu 2024 yameongozwa na kauli mbiu isemayo Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa letu.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa