Mkuu wa mkoa wa Mtwara kanali Sawala amewataka wananchi wa Mkoa wa Mtwara kulinda tunu ya amani katika maeneo yao.
Hayo ameyasema Leo June 24,2024 katika uzinduzi wa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya Mwaka 2022 ambapo mkuu wa Mkoa wa Mtwara amesema bila kuwepo kwa amani hakuna maendeleo kwa jamii au wananchi watakua hawana utulivu wa kuzalisha vyanzo vya kujipatia kupato hivyo ni vema kulinda amani na kuwakataa watu ambao watakuja kwa lengo la kutaka kuvunja utulivu wetu.
Kwaupande wake Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Mhe Abdala Dadi Chikota amesema baada ya mafunzo hayo matarajio yake kuona kwamba wataalamu wa halmashauri na wataalamu wengine wanatumia mafunzo hayo kuandataa taarifa zao za kimaendeleo kupitia idadi ya watu waliohesabiwa na sensa .
Mafunzo hayo yamefanyika Leo kwenye halmashauri ya mji Nanyamba na kujumuisha watendaji,Wenyeviti,Wazee na viongozi mbalimbali wangaza za vijiji na kata.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa