Afisa elimu Halmashauri ya wilaya ya masasi Elizabeth Mlaponi akiongea na walimu wa shule za Msingi Tarafa ya Lulindi kwene mafunzo ya kujengeana uwezo kwenye masomo ya Sayansi, Hesabu na kiingereza ili kuongeza ufaulu
Walimu za shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wameamua kutumia muda wao wa likizo fupi kujengeana uwezo wa mada ngumu kwa masomo ya sayansi, Hisabati na kiingereza lengo ikiwa ni kuongeza ufanisi wa ufundishaji wa masomo hayo na hivyo kuinua ufaulu katika mitihani ya Kitaifa.
Walimu wamefikia hatua hiyo baada ya kuona baadhi ya walimu hawana uwezo wa kufundisha baadhi ya mada kutokana kutokuzielewa vizuri hivyo mafunzo hayo yatawasaidia walimu hao kuwa na uwezo wa kufundisha masomo hayo kwa ufanisi na hivyo kuongeza ufaulu wa masomo hayo.
Akiongea wakati wa mafunzo hayo katika tarafa ya Lulindi wilayani humo, Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Ndugu Elizabeth Mlaponi alisema kuwa mafunzo hayo ni kati mikakati ya kuongeza ufaulu kwa matokeo ya darasa la Nne na la saba kwa mwaka 2018.
Mlaponi alisema kuwa kwa matokeo ya mwaka 2017 masomo ya Kiswahili na maarifa ya jamii ufaulu ulikuwa 50% wakati masomo ya Sayansi, Hisabati na kiingereza ufaulu ulikuwa chini ya asilimia 40 ambapo somo la kiingereza ufaulu ulikuwa chini ikifuatiwa na Hisabati
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa