Halmashauri ya Wilaya Masasi katika kuendana na matumizi ya teknolojia na kupunguza gharama za matumizi ya karatasi katika kusambaza taarifa imeendelea na zoezi la ugawaji wa vishikwambi (tablets) kwa waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri hiyo.
Akikabidhi vishikwambi hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi.Beatrice Mwinuka, Afisa Tehama Bw.Shedrack Mbago Amesema zoezi hilo sio mwanzo bali ni muendelezo wa kile kinachoendelea kwa waheshimiwa Madiwani pamoja na wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali.
" Tupo hapa kwa ajili ya kugawa vishikwambi ambapo vishikwambi hivi ni muendelezo wa matumizi bora na saidizi ya Tehama Katika vikao mbalimbali vya Halmashauri, na ikumbukwe kuwa Halmashauri ilianza matumizi ya Tehama Katika kuendesha vikao vyake tangu Mwaka 2017 mpaka Sasa hivyo kilichofanyika leo sio mwanzo ni muendelezo na matumaini yetu makubwa tunategemea taarifa zote za vikao zitatumwa kwenye vishikwambi hivyo na kuwafikia waheshimiwa Madiwani kwa wakati"..alisema Bw.Mbago
Ameongeza kuwa pamoja na hayo pia wanawapatia mafunzo ya namna bora ya kutimia vishikwambi hivyo.
Nao baadhi ya Madiwani ambao wamepokea vishikwambi hivyo huku wakiwakikilisha wengine wamemshukuru Mkurugenzi pamoja na timu nzima ya Watumishi kwa kufanikisha suala hilo ambapo sasa utendaji wao wa kazi utaimarika zaidi kutokana na matumizi sahihi ya teknolojia hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Masasi ni miongoni mwa Halmashauri nchini ambayo Madiwani wake wameanza kutumia teknolojia katika Shughuli zao za Kila Siku.
29/10/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa