Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Lulindi na Ndanda Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Hadija Mkumbwa ambae alikuwa mgeni rasmi mapema jana tarehe 14 Mei 2025 alifungua rasmi mafunzo ya siku moja kwa Waendesha Vifaa vya BVR (Biometric Voter Registration) pamoja na Waandikishaji Wasaidizi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Bi.Hadija amewataka washiriki kufanya kazi kwa weledi, uadilifu, na kuzingatia kanuni, taratibu na maelekezo yote waliyopewa na Tume ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi na kwa kuzingatia muda uliopangwa.
“Ni matumaini yangu kuwa, kutokana na semina hii kila mmoja wenu atapata elimu ya kutosha itakayomuwezesha kutekeleza majukumu yake ili kufanikisha zoezi hili la kitaifa la uboreshaji wa daftari la wapiga kura". Alisema Bi. Hadija
Aidha ametoa wito kwa washiriki wote kuhakikisha wameyaelewa kwa kina matumizi ya vifaa vya BVR na kuwa tayari kutoa msaada kwa wananch ambao i watahitaji ufafanuzi wakati wa zoezi la uandikishaji ili kuongeza ufanisi na uweledi katika kutekeleza majukumu yao.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwawezesha washiriki kupata ujuzi wa kitaalamu kuhusu matumizi ya teknolojia ya BVR na mbinu sahihi za uandikishaji wa wapiga kura, ili kuhakikisha zoezi linafanyika kwa uwazi, haki na bila changamoto za kiufundi.
Zoezi hilo la uandikishaji wapiga kura awamu ya pili litaanza rasmi siku ya Ijumaa Mei 16 hadi 22 Mei 2025 huku Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ikisisitiza umuhimu wa kila mwananchi kushiriki kikamilifu.
15/05/2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa