Viongozi wa Taasisi za umma Mkoa wa Mtwara wamekumbushwa kuzingatia maadili ya tumishi wa Umma ili kuepusha migongano ya kimaslahi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuhudumia wananchi kama sheria ya maadili kwa viongozi wa Na. 3 ya mwaka 1995 inavyowata kufanya kazi kwa kuzingigatia sheria, kanuni na taratibu.
Hayo yalizungumzwa na Kaimu Katibu msaidizi wa Sekretarieti ya Maadili Kanda ya Kusini ndugu Filotheus Manula wakati wa warsha kwa viongozi wa umma wakiwemo wakuu wa Taasisi, Wakuu wa Idara na viongozi wengine iliyolenga kujenga uelewa wa pamoja katika kutekeleza matakwa ya sheria ikiwemo kuepuka mgongano wa kimaslahi ambalo ndio tatizo kubwa.
“Viongozi wanapaswa kuelewa kuwa mgongano wa kimaslahi ni kinyume na maadili ya viongozi wa umma kwani viongozi wengi wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya yaani kwa maslahi yao na sio kwa maslahi ya umma” kiongozi wa umma nawajibika kwa wananchi na si vinginevyo” alieleza Filotheus.
Manula amesisitiza kuwa ni vizuri viongozi wafanye kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za utumishi wa umma kuonesha utaalamu, uaminifu na uwajibikaji kwani ndio misingi ya utumishi wa umma kama sheria ya maadili ya viongozi wa umma Na.13 ya mwaka 1995 inavyoelekeza.
Akiongea kwa niaba ya washiriki wa warsha hiyo Aliyekuwa Afisa Utumisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ndugu Mohamedi muhidini alisema kuwa warsha hiyo imewasaidia viongozi kutambua nafasi zao kulingana na maadili ya utumishi wa umma ili kutoa huduma bora kwa wananchi
“Tumekumbushwa kuwa waadilifu kama tulivyoapa kuwa waadilifu kwa kufuata misingi ya utawala bora na uwajibikaji na sio kutumia nafasi zetu kwa maslahi binafsi” alieleza Mhidini.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa