Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimisha Gelasius Byakanwa amewasimamisha kazi baadhi ya Viongozi wa Vyama vya ushirikika Wilaya za Masasi na Nnanyumbu Mkoani Mtwara waliokosa sifa za kuendelea kufanaya kazi kwenye vyama hivyo ikiwemo waliosababisha madeni ya wakulima kwa msimu wa 2017/2018.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mhe Juma Satmah akitoa neno mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa wakati wa kikao cha viongozi wa AMCOS kilicholenga kufanya tathimini ya mwenendo wa msimu wa korosho kwa mwaka 2017/2018
Byakanwa amewasimamisha kazi viongozi hao leo wakati wa kikao cha tathimini ya mwenendo wa uuzaji wa zao la korosho kwa msimu wa 2017/2018 mkoani humo na kuweka mipango kwa ajili ya msimu mpya wa korosho 2018/2019 ambapo unategemewa kuwa msimu ambao hautasababisha madeni ya malipo ya korosho kwa wakulima kwani kila mdau atapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na sheria zilizopo.
Viongozi wakifuatilia kwa makini kikao cha tathimini ya mwenendo wa msimu wa korosho kwa mwaka 2017/2018
Akiongea kwenye kikao hicho, Byakanwa alieleza kuwa matatizo mengi ya korosho katika msimu wa korosho uliopita yalisababishwa na viongozi wa vyama vya Ushirika kutotekeleza wajibu wao wa uadilifu ambapo baadhi walifanya ubadhilifu kwa makusudi, wizi wa fedha za wakulima, uzembe, na uelewa mdogo wa kuendesha vyama hali iliyopelekea wakulima wengi kutolipwa fedha zao.
“Tulisema wasiokuwa na sifa za kufanya kazi kwenye vyama vya ushirika waondolewe na sasa tunatekeleza, msimu ujao hautakuwa na matatizo “ alisema Byakanwa.
Kiongozi wa Amcos akieleza chanagamoto wananzokutana nazo zinazochangia matatatizo kipindi cha Msimu katika kikao cha tathimini ya mwenendo wa msimu wa korosho kwa mwaka 2017/2018
Kwa msimu 2017/2018 Mkoa ulifanya jitihada za kuhakikisha wakulima wanaodai fedha zao za korosho wanalipwa ambapo viongozi wa vyama vya ushirika ambavyo havikuwalipa wakulima fedha zao walichukuliwa hatua za kisheria na kuhakikisha wanalipa madeni hayo kwa kuuza mali zao ikiwemo mashamba na nyumba.
Aidha Byakanwa amewasisitiza viongozi watakaoendelea kufanya kazi kwenye vyama vya ushirika kwa msimu huu mpya 2018/2018 kuhakiksha makosa yaliyojitokeza katika msimu wa 2017/2018 hayatokei, hivyo wanapaswa kufanya kazi wa uadilifu mkubwa kwani Mkoa hauko tayari kuona wakulima hawalipwi malipo yao.
Ili kuhakikisha msimu mpya wa korosho unaendeshwa vizuri, Mkuu wa Mkoa amejipangia utaratibu wa kufanya vikao na kuwekeana mikakati na wadau wote wa korosho wakiwemo viongozi wa vyama vya ushirika, vyama vikuu, mabenki na wamiliki wa maghala ya kuhifadhia korosho ili kuhakikisha biashara ya korosho inaenda vizuri hasa kuhakiksha mkulima anapata haki yake kwa wakati.
Viongozi wakifuatilia kwa makini majadiliano kwenye kikao cha tathimini ya musimu wa korosho 2017/2018
Kwa upande wao viongozi wa Vyama vya ushirika wamempongeza Mkuu wa Mkoa kwa jitihada zake za kuhakiksha viongozi waliosababisha madeni kwa wakulima wanachukuliwa hatua za kisheria za kuhakikisha wanarejesha fedha zote zilizopotea na kuwalipa wakulima jambo ambalo halijawahi kufanyika katika misimu ya nyuma.
“Kuna wakulima ambao hawakulipwa fedha zao kwa misimu ya nyuma lakini hakukuwa na jitihada zozote zilizofanyika kuhakikisha viongozi wabadhirifu wanarejesha fedha na kuwalipa wakulima , tunampongeza sana”
Viongozi wakifuatilia kwa makini majadiliano kwenye kikao cha tathimini ya musimu wa korosho 2017/2018
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa