Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bibi Changwa Mkwazu akiwa na baadhi ya wakuu wa idara amekutana na kufanya kikao cha awali na mwekezaji “Malaika Construction Company” anayetarajia kuwekeza katika vitalu vya uchimbaji wa madini ya ujenzi vinavyomilikiwa na halmashauri hiyo katika kijiji cha chipite.
Baada ya kikao hicho kilichofanyika leo tarehe 19.08.2020 kwa pamoja wamekubaliana kuwa uwekezaji huo utakuwa ni wa mkataba kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi na kamuni ya ujenzi ya Malaika “Malaika Construction company” ambapo halmashauri itaendelea kuwa mmiliki wa vitalu hivyo na itapata faida si zaidi ya asilimia 40 kwa kuwa mwekezaji atatekeleza majukumu mengi zaidi .
Aidha katika mkataba huo mwekezaji atawajibika kutoa gharama zote za uendeshaji ikwemo kuweka mitambo na nguvu kazi pamoja na kuwajibika na mashariti mengine ya kimkataba ikiwemo kuwa na mkakati wa kutunza mazingira, na kushirikiana na jamii katika shughuli za maendeleo.
Pia Mkwazu ameeleza kuwa, mpaka sasa Halmashauri inawawekezaji watatu wanaofanya kazi ya uchakataji wa madini ya ujenzi katika vitalu vinavyomilikiwa na watu tofauti kwenye eneo la chipite kata ya nanganga, huku Halmashauri ikiwa na umiliki wa vitalu 6 pekee
"Uwekezaji unaofanyika kwenye madini ya ugenzi unachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza mapato anayofanikisha uendeshaji wa shughuli mbalimbali ikiwemo uteelezaji wa miradi ya maendeleo, nitumie fursa hii kuwa karibisha wawekezaji wengine kuja kuwekaza katika Halmashauri yetu kwani maeneo ya uwekezaji bado ni mengi sana" ameeleza Mkwazu.
Madini ya ujenzi yanayozalishwa katika vitalu vya eneo la Chipite hususani kokoto zimethibishwa kuwa ni zenye ubora wa kiwango cha juu na zinafaa sana kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo viwanja vya ndege, barabara na majengo makubwa.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa