Ushirikiano kati ya Halmashauri za wilaya ya Masasi (Mji na wilaya) umekuwa wa mafanikio makubwa hasa kwa wananchi wa masasi kutokana na miradi mbalimbali inayotekelezwa kulenga kuboresha huduma kwa wananchi na watumishi katika wilaya ya masasi ambapo masuala ya afya , elimu na mazingira yanapewa kipaumbele katika ushirikiano huo.
kutokana na mashirikiano hayo wawakilishi kutoka Ujerumani wamekuja na kufanya kikao kinacholenga kujadili utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea na iliyokamilia pamoja na mipango madhubuti ya kuendeleza ushirikiano huo ambapo kwa sasa wanatarajia kuanzia biashara ya korosho za masasi kwenda ujerumani pamoja na kujenga hotel ya pamoja
Katika ushirikiano huo halmashauri za Masasi wamefanikiwa kutekeleza Miradi mbalimbali ikiwemo uwekaji wa umeme jua kwenye kituo vya kutolea Huduma zaafya, matumizi ya nishati mbadala (Bayogas) na masuala ya Elimu ambapowanafunzi wa shule ya wasichana Ndwika wamekuwa na ziara za mafunzo katikashule za Enzkreis.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa