Halmashauri ya wilaya masasi mkoani mtwara imedhamilia kudhibiti vifo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5 vinavyosababishwa na ukosefu wa chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya surua na polio kwa kutoa huduma hiyo kwa watoto kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kwa njia ya huduma ya mkoba ambapo wataalamu wa zahanati wanawatembelea watoto kwenye maeneo yasiyo na huduma ya afya.
Hayo yalisemwa na mgeni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo bibi changwa M. mkwazu wakati wa kufungua warsha ya watoa huduma ya chanjo kwa watumishi wapya wa idara ya afya kilichofanyika tarehe 20.02.2017 iliyolenga kuwajengewa uwezo watumishi hao juu ya utoaji mzuri wa huduma za chanjo katika ngazi ya jamii.
Mkwazu amesema “Halmashauri yetu tumeamua kuandaa warsha ya kuwajengea uwezo watumishi wa wapya jinsi ya kuboresha huduma za chanjo ambapo kila mtoto afikiwe na huduma ya hii ili utoaji wa huduma hii upande kutoka asilimia 99 ya sasa na kufikia zaidi ya asilimia 100.
Watoto walio na umri chini ya mwaka mmoja wakipata Chanjo wanakingwa dhidi ya magonjwa 11 yanayozuilika kwa chanjo na magonjwa hayo ikiwa ni pamoja kifua kikuu, kifuaduro, dondakoo, pepopunda, surua, Rubella ,polio, Homa ya uti wa mgongo, Kuhara, Nimonia pamoja na Homa ya ini.
Kwa maana hiyo chanjo ni muhimu sana kwani zinahakikisha mtoto anakuwa na kinga ya magonjwa mbalimbali katika maisha yake yote ambayo mengine hayana dawa, chanjo ni jambo la lazima kila mtoto ni lazima apate chanjo zote zilizopendekezwa katika mwaka wa kwanza na wa pili hivyo wazazi wote au walezi wengine wanapaswa kuzingatia ushauri wa mtaalamu wa afya kuhusu muda wa kukamilisha chanjo zinazohitajika.
Jamii yetu ya Tanzania inabidi tuache imani potofu juu ya kukwepa chanjo kwa kuhofia kuwa zina sumu, kufanya hivyo unaweka maisha ya mtoto hatarini iwapo umetokea ugonjwa wa mlipuko kupona kwake ni ngumu sana na akipata maradhi tu yoyote uhai wake upo mashakani
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa