Mhe. WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani ameeleza kuwa, serikali kupitia mradi wa REA III unaotekelezwa nchini imedhamilia kuweka umeme nyumba kwa nyumba kuanzia nyumba ya nyasi hadi ya ghorofa kwa gharama ya shilingi 27,000 tu.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mpeta wilayani masasi wakati wa ziara yake mkoa wa Mtwara, alisema kuwa Serikali pamoja na watalaamu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na REA wamekuwa wakifanyakazi usiku na mchana ili kuhakikisha kazi ya uunganishaji umeme inafanyika kwa haraka ili wananchi wapate umeme na pia kuchochea uanzishwaji wa viwanda
Mhe. Kalemage amewahakikishia wananchi kuwa “wewe mwananchi sema unataka uunganishiwe umeme wapi iwe kwenye nyumba ya majani, tembe, makuti au ghorofa zote zitawekewa umeme, haturuki nyumba na nitasimamia”
Mwananchi atalipia shilingi 27,000 kwa ajili ya kuunganishiwa umeme ila gharama za kuweka miundombinu ya ndani (wiring) itakuwa nje ya fedha hiyo, ili kupunguza gharama mwananchi anaweza kununua kifaa ambacho hakihitaji kuweka miundombinu ya ndani.
Ili kuwezesha zoezi la uunganishaji wa umeme kwa haraka Mhe. waziri amewaagiza kuweka ofisi ngazi ya kata ili kuwarahisishia wananchi kulipia gharama za kuunganishiwa umeme kwenye kata badala ya kwenda Ofisi za makao makuu hali ambayo inaongeza gharama kwa wananchi.
Aidha, Dk. Kalamage amewaeleza wananchi kuwa wanaweza kulipia kidogo kidogo gharama za kuunganishiwa umeme na pindi wanapofikisha Shilingi 27,000 wataunganishiwa huduma hiyo, lengo la serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata umeme ndani ya kipindi cha mradi.
Wakiongea mbele ya Mhe. Waziri, wananchi wa mpeta wameishukuru serikali kwa kupeleka huduma ya umeme vijijini maana ni huduma muhimu kwani itasaidia kuanzisha shughuli mbaimbali za kiuchumi na hivyo kuboresha maisha yao.
Aidha Dkt. Kalemani amewataka watanzania kuchangumkia fursa ya kuunganishiwa umeme kwa kutumia kifaa kinachojulikana kama Umeme Tayari (UMETA) kwani mtumiaji hatatakiwa kuweka miundombinu ya umeme yaani wiring na hivyo kupunguza gharama za kuunganishiwa umeme kwa matumizi ya nyumbani sio viwandani.
Mhe. Waziri ameshauri kuwa kutokana na urahisi wa kifaa hichi nashauri kitumike kwenye majengo ya taasisi za Umma ikiwemo ofisi za vijiji kata, vituo vya afya , zahanati, vituo vya polisi, na maeneo mengine ambayo hayana ulazima wa kuweka miundombinu ya umeme yaani wiring.” Kwani garama yake ni shilingi 36,000 tu.
Mradi wa REA III kwa mkoa wa Mtwara ulizinduliwa Agositi mwaka 2017 ambao kwa Wilaya ya Masasi vijiji 52 vitaunganishwa
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa