UJENZI WA JENGO LA WAGONJWA WA NJE (OPD) NAMWANGA LAWEKWA JIWE LA MSINGI.
Mwenge wa uhuru 2024 umetembelea, kukagua na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa jengo la utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD) la kituo cha Afya Namwanga .
Mradi huu ambao unatekelezwa kwa njia ya "Force account"kwa kutumia Local fundi, kazi zilizofanyika mpaka sasa ni ujenzi wa boma, kuezeka/upigaji wa bati na Blunering, kupiga lipu/plasta na uwekaji wa Grill za madirisha.
Aidha mradi huu ukikamilika unategemea kutoa huduma yenye ngazi ya kituo cha Afya kwa Wananchi waishio kata ya Namwanga na kata jirani kama vile Mkululu,Mpindimbi, Mijelejele ambapo jumla ya wakazi 28,218 watanufaika.
Akiweka jiwe hilo la msingi jana june 05,2024 katika jengo hilo ambalo linatarajiwa kuwa kituo cha Afya, kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2024 Ndg.Godfrey Eliakimu Mzava amesema, katika eneo hilo wamepokea taarifa ya mapambano dhidi ya Malaria, mapambano dhidi ya Ukimwi, mapambano dhidi ya madawa ya kulevya pamoja na taarifa ya utekelezaji wa mradi wa jengo la utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa nje ( OPD) cha zahanati ya Namwanga ambayo ina mpango wa kuwa kituo cha Afya .
Amesema katika maeneo hayo yote wameona yapo vizuri ila katika eneo la mapambano dhidi ya Malaria yapo maagizo ya mhe.Rais kuhusu ununuzi wa dawa za viua dudu ambazo zitatumika katika kutokomeza Malaria,maelekezo yanaelekeza Halmashauri itenge fedha kutoka mapato ya ndani kwenda kununua dawa ya viua dudu na baadaye wainishe maeneo ambayo yana mazalia ya mbu ili waje kupulizia ikiwa ni moja ya mkakati madhubuti wa kupambana na malaria .
Aidha amesema pamoja kwamba agizo hilo bado utekelezaji wake haujakamilika lakini wamepata ahadi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Masasi ambaye pia ndiye Mganga mkuu Dkt.Ruben Mwakilima kwamba kabla ya tarehe 15 watakwenda kuchukua hiyo dawa ikiwa kwasasa wana lita 5 tu zimenunuliwa fedha kutoka kwenye mfuko wa wahisani na wafadhili mbalimbali kutoka sekta ya Afya.
Hata hivyo ifahamike kuwa kata ya Namwanga imepokea fedha kwa awamu mbili kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje OPD la kituo cha Afya, ambapo shilingi Milioni 50 awamu ya kwanza tarehe 07/02/2023, awamu ya pili milioni 25 tarehe 06/3/2024 na kufanya jumla ya tsh.77,025,025 na mchango wa wananchi Tshs.milioni mbili ishirini na tano elfu na ishirini na tano ikiwa ni kutoa eneo la ujenzi lenye ekari 15,usafi wa eneo la ujenzi, kuweka kifusi kwenye msingi wa jengo na ulinzi wa vifaa.
Kazi iendeleee.....
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa